WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WAIANGUKIA SERIKALI KUWAPATIA RUZUKU

Mchimbaji mdogo wa madini Rachel Njau akizungumza kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji wakati wa uchangiaji mada ya urasimishaji wachimbaji wadogo kwenye sekta ya uziduaji, na kuimba Serikali iwawezeshe ikiwamo kuwapatia Ruzuku.

Mjadala ukiendelea wa kurasimisha sekta ya uchimbaji mdogo.

Na Marco Maduhu, DODOMA

WACHIMBAJI wadogo wa madini hapa nchini wameiomba Serikali iwe inawapatia Ruzuku na kupata mitaji ya kununua dhana za kuendeleza uchimbaji huo, ili kuinuka kiuchumi pamoja na kuchangia pato la Taifa.

Wamebainisha hayo leo kwenye Jukwaa la Sekta ya uziduaji lililoandaliwa na HakiRasilimali, wakati Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo hapa nchini FADev ilipokuwa ikiongoza mjadala wa Serikali kurasimisha sekta ya uchimbaji mdogo.

Wamesema Serikali inapaswa kuwashika mkono wachimbaji wadogo ili wainuke ikiwamo na kuwapatia Ruzuku, na siyo kuwasukumia kwenye Taasisi za kifedha (benki) mahali ambapo hawawezi kukopesheka.

"Serikali kupitia Wizara ya Madini tunaiomba itupatie Ruzuku wachimbaji wadogo na siyo kutusukumia kwenye mabenki ambayo hayawezi kutupatia mikopo," amesema Rachel Njau.

Aidha, Mchimbaji Pili Husein kutoka Mererani ametoa ushuhuda namna alivyonufaika na Ruzuku ya Serikali Sh.milioni 80 ambayo aliipata mwaka 2013, anasema ili msaidia sana kumkuza katika sekta hiyo ya uchimbaji mdogo, huku akiiomba Serikali kuendelea kutoa ruzuku hizo kwa wingi.

Naye Kamishna Msaidizi kitengo cha wachimbaji wadogo kutoka Wizara ya Madini Francis Mihayo, amesema Serikali iliweka utaratibu wa kuwapatia Ruzuku wachimbaji wadogo, lakini baadhi yao wakawa wanazitumia fedha hizo kinyume na matarajio ndipo ikabidi wasitishe kwanza.

"Mwaka 2013 Serikali iliweka utaratibu wa kuwasaidia wachimbaji wa wadogo mara baada ya kuitambua fursa ya madini pamoja na kuwapatia Ruzuku, lakini unampatia mtu Ruzuku akanunue Roli la kubeba vifusi ya udongo wa madini ana kwenda kununia Kirikuu, mwingine badala ya kununua pampu ya kuvuta maji mgodini anunua pampu ya nyumbani," anasema Mihayo.

Kwa upande Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, amesema Serikali pamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali zinapaswa kuwashika mkono wachimbaji wadogo pamoja na kuwapatia elimu na kutambua uchimbaji ni kama biashara zingine na wanamchango mkubwa katika pato la Taifa.

Amesema wao kama Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo, wameshaunda vikundi 15 vya wachimbaji wadogo na kuwapatia Ruzuku, pamoja na wengine kuwaunganisha kwenye Taasisi za kifedha ili wapate kukopesheka, na kuwapatia pia elimu namna ya kuhifadhi taarifa zao za kibenki.

Naye Prof Abel Kinyondo kutoka Chuo Kikuu cha Da er Salaam, anasema Urasimishaji wa Sekta hiyo usajili ni kati ya vitu vingi ambavyo vinapaswa kutokea, ikiwamo wachimbaji kupewa elimu ya kufanya uchimbaji ambao ni rafiki kwa afya na mazingira, wawe kitaasisi zaidi, kuwawezesha kufikia huduma za kifedha ili wakopesheke.
Pamoja na kuongeza matunzi ya Teknolojia ambayo ni bora zaidi, lakini mambo hayo hayawekewi msingi mzito.
Meneja Program na utafiti kutoka FADev Evans Rubara akiongoza mjadala wa Urasimishaji sekta ya uchimbaji mdogo.

Mjadala ukiendelea wa kurasimisha sekta ya uchimbaji mdogo.

Uwasilishaji wa mada ya namna gani Afrika inaweza kunufaika kuhusu mhamo wa nishati.

Mjadala ukiendelea kwenye jukwaa hilo la sekta ya uziduaji.

Mjadala ukiendelea kwenye jukwaa hilo la sekta ya uziduaji.

Wadau wakiendelea kusikiliza mijadala mbalimbali katika jukwaa la sekta ya uziduaji.

Mchimbaji mdogo wa madini Rachel Njau akichangia mjadala kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Mchimbaji mdogo wa madini Pili Husein akichangia mjadala kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Sheikh wa Mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi akichangia mjadala kwenye jukwaa la sekta ya uziduaji.

Wadau wakiendelea kusikiliza mijadala mbalimbali katika jukwaa la sekta ya uziduaji.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464