Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumzia miradi ya Maendeleo ya hslmashauri ya wilaya hiyo
Suzy Luhende,Shinyanga blog
Kishapu. Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude amesema Zaidi ya sh 20 bilioni kutekeleza miradi mbalimbali ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambazo vyanzo vikubwa vya fedha hizo ni kutoka serikali kuu, ikiwa kipaumbele cha wilaya hiyo ilikuwa ni sekta ya elimu.
Hayo ameyasema hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake, ambapo amesema fedha hizo zimekamilisha miradi mbalimbali yakiwemo madarasa, zahanati vituo vya afya, hosipitali ya wilaya ya Kishapu, barabara na maji
Mkude alisema kutokana na fedha hizo tayari madarasa yamekamilika na sasa mengine yanatumika na mengine yanasubiri watoto wa kidato cha kwanza, hivyo watoto wote watakaofaulu kuongia kidato cha kwanza hawatapata shida wote wataingia darasani hakuna atakayebaki.
"Madarasa yote yamekamilika asiwepo mzazi wa kusafirisha mtoto ama wakuozesha mtoto, kwa kisingizio madarasa, watoto wote watakaofaulu waripoti mashuleni kwa wakati ili kuweza kuendelea na masomo sisi wazazi tusiwadanganye watoto kukaa nyumbani ,"alisema Mkude.
Mkude alisema kwa sasa wanaendelea kutekeleza ujenzi wa vyoo na matundu yake, ili kuhakikisha shule zote zinakuwa na vyoo vya kutosha wanafunzi wasipate shida.
"Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu ameweka kipaumbele katika sekta ya elimu, elimu bure kuanzia chekechea hadi sekondari na kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo wenye sifa zinazotakiwa, hivyo ameonyesha njia ni sisi tu, hivyo wananchi wanaishukuru sana serikali kwa kuwajali "alisema Mkude.
Wilaya ya Kishapu ina mgodi wa almasi ambapo hivi karibuni serikali imesaini mkataba kati ya halmashauri na mgodi wa almasi Mwadui kampuni ya Williamson Diamond (WDL) ambapo unailipa halmashauri ya wilaya sh 1.2 bilioni sawa na asilimia 0.7 ambapo huko nyuma kulikuwa na hisa chache kabla ya mkataba huu ilikuwa ikilipwa sh 150 milioni.
"Kwa kweli mabadiliko haya yataleta maendeleo kwa wananchi kwani fedha hizi zitanufaisha kata tano na vijiji 19 vinavyozunguka mgodi na kutakuwa na miradi ya aina tatu kuanzia ngazi ya vijiji,Kata na miradi itakayosimamiwa na Wilaya ili kuwaondolea changamoto wananchi,"alisema Mkude.
Mkude alisema hivi karibuni pia wamepokea fedha kwa ajili ya kujenga ofisi ya mkuu wa wilaya sh 1.6 bolioni ambazo zinajenga jengo aina ya gorofa, pia wamepokea fedha Sh 300 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya na tayari majengo yote yanaendelea kuboreshwa.
"Tunaishukuru sana serikali ya mama yetu mama samia Suluhu kwa kuweza kutujali na kuwajali wananchi wake kwani hata sekta ya elimu imeajili walimu wa kutosha katika wilaya yetu ili watoto waweze kutundishwa na kupata elimu bora na kuweza kufaulu vizuri"alisema Mkude.
Mkude alisema licha kupata mafanikio makubwa pia amewamba wananchi kulima mazao yanayositahimili ukame mtama,choroko na mazao mengine ya biashara pamba Arizeti na mahindi ili kuondokana na janga la njaa, pia amesisitiza kuwa mvua zinapoanza kunyesha wananchi wajitokeze mapema.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kishapu Astelia Joseph na Masanja Jima walisema wanaishukuru sana serikali kwani watoto wengi walikuwa wanasoma chini ya miti lakini kwa sasa kuna madarasa ya kutosha, pia zahanati zipo za kutosha na zingine zinamaliziwa kujengwa, hivyo kina mama wajawazito hawatajifungulia barabarani kama awali.
"Tnaishukuru sana serikali kwa kutukumbuka hata kwenye barabara kwani tulikuwa tukipata shida kubwa hata maji serikari inaendelea kuboresha vijiji kadhaa vimeshapata maji ya ziwa victoria, hivyo na vingine vinae delea kuboreshewa ili kuhakikisha kila kata inapata ma ikiwa ni pamoja na umeme,"alisema Luhende Nyangindu mkazi wa kijiji cha Lagana.
Jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu likiendelea kujengwa
Jengo la chuo cha Veta Kishapu
Kazi inaendelea katika chuo cha Veta Kishapu vifaa mbalimbali vinaendelea kupelekwa vikiwemo meza na viti kwa ajili ya wanafunzi watakaoanza katika chuo hicho
Wanafunzi wa chuo cha Veta wakiangalia mazingira ya chuo hicho yalivyo kaa
Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Kishapu wakisikiliza mkuu wa wilaya akisoma taarifa ya utekelezaji wa maendeleo
Mkuu wa wilaya ya Kishapu akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo