ALUWA MKILINDI : KILA MTU ANA JUKUMU LA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

 Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) umeendesha Mdahalo uliokutanisha Wajumbe wa kamati za Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto kwenye vijiji na kata ya Shilela, viongozi wa serikali za vijiji na kata pamoja na Wana Jamiii uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa Mdahalo huo uliofanyika leo Jumatatu Desemba 19,2022 katika kijiji cha Shilela kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga,   Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi amesema suala la kupinga ukatili wa kijinsia halitakiwi kuwa la mtu mmoja bali ni lazima kila mmoja ashiriki kutokomeza ukatili ili jamii iishi kwa amani.

“Kila mmoja kwa nafasi yake, ashiriki kumaliza ukatili wa kijinsia, wanawake wapewe fursa ya kumiliki rasilimali, wajane wasinyanyaswe, watoto wapelekwe shule badala ya kuozeshwa wangali wadogo,mila zinazomkandamiza mwanamke ziachwe, Waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi waachane na ramli zinazochochea ukatili wa kijinsia”,amesema Mkilindi.

Nao washiriki wa Mdahalo huo akiwemo Amos Daudi Bakundikija, Esther Saleh Kazonzola, na Boniphace Machurya wamesema hatua kubwa zimefikiwa katika kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Taarifa na Maarifa kinachosimamiwa na TGNP kata ya Shilela ni pamoja na kupungua kwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni,kurithi na kunyanyasa wajane.

Aidha wamesema bado kuna uoga au siri kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia hali hii inayosababisha ukatili wa kijinsia kuendelea kujitokeza huku wakishauri kuendeleza Mila zitakazosaidia kuondoa ukatili wa kijinsia.

“Pia tunatakiwa kuendelea kutunza siri za watu wanaotoa taarifa za ukatili wa kijinsia, kuongeza vituo vya unasihi na misaada ya kisheria,uwajibikaji wa jamii, Uundwaji wa sheria ndogo zitakazotubana kuachana na ukatili wa kijinsia na tuwe na nguvu ya pamoja katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia”,wameongeza.
 Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
 Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Viongozi na wanajamii wakiwa kwenye mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela, Mwanaidi Mustapha Mzee akizungumza kwenye mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala 
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Joseph Mbunge  akizungumza kwenye mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Shilela Deogratius Nkwabi akizungumza kwenye mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala 
Viongozi na wanajamii wakiwa kwenye mdahalo uliolenga kujadili mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464