Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP, Janeth Magomi
NA HALIMA KHOYA, SHINYANGA.
Mkazi wa Butengwa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Richard Nzumbe amefariki dunia kwa kudaiwa kuvamiwa na majambazi na kupigwa Risasi akiwa anaingia nyumbani kwake.
Tukio hilo la uvamizi kwa kutumia silaha uliosababisha kifo cha Richald Nzumbe,limetokea Desemba 19,2022 majira ya saa 1 usiku katika Kata ya Butengwa Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.
Akieleza juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa Butengwa,Onesmo Mayeba,Amesema majira ya saa 1 usiku alipewa taarifa na mwananchi juu ya tukio hilo ambapo alifika eneo husika na kukuta majambazi hao wamekwisha tenda uvamizi huo huku ikisemekana lengo la kufanya uvamizi huo ni kuwania fedha kutoka kwa marehemu Richald.
“Tukio hili ni lakikatili na tunalilaani kwa sababu majambazi hawa wametoa uhai wa mtu ambapo ni kosa la jinai,hivyo tunaliomba jeshi la polisi kuwabainisha wote waliohusika kutenda mauaji hayo na kuwapa adhabu kulingana na Sheria”Amesema Mayenda.
Awali akieleza undani wa tukio hilo Shemeji wa marehemu,Salome Dady, amesema majira ya saa 1 usiku walikuwa ndani yeye na watoto wa dada yake,ndipo waliposikia gari la shemeji yake likiwa limefika getini ambapo mtoto wake alienda kufungua geti hilo ndipo aliposukumwa na majambazi hao na kumfuata marehemu kisha kumfanyia unyama huo.
"Tulikuwa ndani mimi na watoto wa dada mara tukasikia gari likiwa getini ambapo alienda mtoto wa dada kufungua mlango ndipo nikasikia kelele nje ikabidi nitoke nikaone kuna nini nikakuta watu wawili wanampiga risasi shemeji ikabidi nichukue stuli nikampiga mmoja akaanguka alafu nikaenda kuchukuq kisu nikamchoma nacho mwingine ndo wakachukuana wakaondoka"Amesema Salome Dady.
Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi Amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema cmJeshi la polisi linaendelea na msako wa kina kuwabainisha waliohusika na tukio hilo