BAADHI
YA WAZAZI NA WALEZI WA KATA YA MWAKITOLYO KUZUIA WATOTO KUPATA ELIMU
Na
Mwandishi wetu.
Waalimu wa shule za msingi katika kata ya Mwakitolyo wamelalamikia
baadhi ya wazazi na walezi kuwanyima
haki ya msingi ya elimu watoto wao kwa kuwatumikisha kwenye shughuli mbalimbali
za familia bila kutambua umuhimu wa elimu.
Waalimu hao wa kata ya
Mwakitolyo wameieleza Shinyanga Press Club blog ilipotembelea kata ya
Mwakitolyo ikiwa na lengo la kungalia hali ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya
eneo hilo.
Baadhi ya wazazi na walezi ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamekuwa na vitendo vya kuwanyima watoto wao haki ya elimu kwa kuwatumikisha shughuli za ufugaji,kilimo,madini na kulea watoto.Aidha uelewa mdogo, mila na desturi imeelezwa kuwa chanzo cha kuwanyima watoto haki ya elimu.
Frank Medembo, Mwalimu
Mkuu Msaidizi katika shule ya Msingi Mwakitolyo anasema kuwa wazazi wamekuwa
wakitumia sababu zisizo na mashiko za kuomba ruhusa ili kwenda kuwatumikisha
watoto katika shughuli mbalimbali.
Pia mwalimu Zubeda Mohamed wa darasa la tatu shule ya msingi Mwakitolyo alisema,wazazi kufika shuleni na kuomba ruhusa ya watoto wao wabaki majumbani ili wao waende gulio au mke wangu amejifungua hivyo mtoto akasaidie mama yake kazi.
“Uchimbaji ni
chamgamoto kubwa sana kwa sababu kuna vishawishi vingi kwa watoto wa kike kwa
kukutana na wavulana ambao wako katika uchimbaji na kusababisha mimba na kuacha
shule” Alisema Zubeda.
Dina Pius mwanafunzi wa
darasa la sita wa shule ya msingi
Mwakitolyo,alieza kuwa wazazi na walezi kuwafanyia ukatili watoto
wenzake kwa kuwanyima kufika
shule na kuwapa kazi majumbani.
“Aina za ukatili wanaofanyiwa watoto ni utoro shuleni,
kufanyishwa kazi, kuponda mawe,kufanya kazi za hotelini na maduarani ili
watafute hela”Alisema Dina
Naye mtendaji wa kata
ya Mwakitolyo,Lutemba Butonja alisema,Watoto wengi wanajua wakienda kuchimba
wanapata fedha na hivyo wanaamini wakisoma hawawezi kupata fedha,ambapo anasema
kuwa suala hilo limedhibitiwa.
“Tumejitajidi sana
kuthibiti hili kwa kuhakikisha kwamba tunafata sheria ya kutumikisha watoto
,tusimwone chini ya miaka 18 mtoto anafanya kazi na shughuli za uchimbaji,kama
serikali tumekuwa tukisimamia sana na kuwapa elimu kwa wale watu wanao ajiri
watoto kwa kufata sheria kuwa hairuhisiwi kuajiri mtoto chini ya miaka 18 na hii
imetusaidia sana”