WAANDISHI WA HABARI, WAENDESHA BAISKELI WAPEWA ELIMU RUSHWA YA NGONO

 
Mkurugenzi wa Shirika la karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Karibu Tanzania Organization (KTO), kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija (FDC), pamoja na Takukuru,wametoa elimu ya Rushwa ya ngono kwa Chama cha waendesha Baiskeli na Waandishi wa habari mkoani Shinyanga ili wakasambaze elimu hiyo kwa jamii.

Elimu hiyo imetolewa leo Desemba 16,2022 katika ukumbi wa mikutano katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Shirika la KTO Maggid Mjengwa, amesema Shirika hilo wamekuwa wakifanya kazi na vyuo vya maendeleo ya wananchi, kutoa elimu ya Rushwa ya ngono.

Amesema mwaka 2005, Shirika hilo walikumbana na kazia katika chuo kimoja cha maendeleo ya wananchi, Mkuu wake wa Chuo kutumia Madaraka vibaya kwa kuomba Rushwa ya ngono kwa wanafunzi, ndipo wakaona kuna umuhimu wa kutoa elimu hiyo katika vyuo vya maendeleo.

Amesema baada ya kutoa elimu hiyo ya Rushwa ya ngono katika vyuo vya maendeleo, wakaona wapanue wigo ili kuifikisha elimu kwa jamii pia kupitia Chama cha waendesha Baiskeli, pamoja na waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao.

"Waendesha Baiskeli huwa wanafikia watu wengi sana, pamoja na waandishi wa habari hivyo tuna imani elimu hii ya Rushwa ya ngono itasambaa katika maeneo mengi na kuifikia jamii,"amesema Mjengwa.

Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija FDC mkoani Shinyanga Maria Mkanwa amesema Rushwa ya ngono imekuwa ikinyima fursa kwa watu wengi hasa wanawake na watoto wa kike, na katika Chuo hicho wamekuwa wakipokea watoto ambao walikatishwa masomo kwa kupewa ujauzito ikiwamo sababu ya Rushwa ya ngono.

Kwa upande wake Afisa uchunguzi kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga Reuben Chongolo, akitoa elimu hiyo ya Rushwa ya ngono amesema chanzo chake kikubwa ni Mmonyoko wa maadili pamoja na wenye Mamlaka kutumia madaraka yao vibaya.

Amesema ili kukabiliana na Rushwa hiyo ya ngono, kitu cha msingi ni kusimama kwenye misingi ya uadilifu, huku akibainisha madhara ya Rushwa ya ngono ni kupoteza utu wa mtu, kukosa fursa, mimba zisizo tarajiwa, pamoja na kupata magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi.

Naye Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja, amelipongeza Shirika hilo la KTO, kwa kuendesha programu hiyo ya kutoa elimu ya Rushwa ya ngono, na kuisambaza pia kwa jamii kupitia vyombo vya habari ambayo vinafikia wananchi wengi.

"Waandishi wa habari, waendesha Baiskeli pamoja na wananchi wote, sote tuungane tukatae Rushwa ya ngono," amesema Mwamba.

Aidha Shirika hilo la Karibu Tanzania Organization (KTO) kesho Desemba 17,2022 litazindua Rasmi elimu ya utoaji Rushwa ya ngono hapa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage na Kampeni hiyo ina Kauli Mbiu isemayo, kuwa jasiri Kataa Rushwa ya ngono.
 
Mkurugenzi wa Shirika la karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija FDC Maria Mkanwa, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Naibu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Shinyanga akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 
Afisa uchunguzi kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga Ruben Chongolo akitoa mafunzo ya Rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari na Chama cha waendesha Baiskeli.
Afisa Habari wa Shirika la Karibu Tanzania Organization Bi. Symphrose Makungu akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.
 
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waendesha Baiskeli wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waendesha Baiskeli wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waendesha Baiskeli wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.

 
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waendesha Baiskeli wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waendesha Baiskeli wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Rushwa ya ngono.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464