Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesh Bunduki aina ya Gobore ambayo wameikamata katika msako.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limekamata vitu mbalimbali vya wizi, pamoja na bunduki na madawa ya kulevya, huku likieleza kuwatia mbaroni baadhi ya watuhumiwa wakiwamo na wabakaji kuhukumiwa kuchapwa viboko na kufungwa Jela.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo Desemba 19, 2022, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya msako ambao wameufanya kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Novemba 22 hadi Desemba 12 mwaka huu.
Amesema katika msako huo wamekamata vifaa tiba vya zahanati ya Uyongo halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Bunduki moja aina ya Gobore, simu za mkononi 17, Pikipiki 10, dawa za kulevya Heroine 10, Bangi kete 71, Tv Nne, Mitungi ya Gesi miwili na lita 20 za Gongo.
Ametaja vitu vingine ambavyo wamevikamata kuwa ni vyuma vya ujenzi wa minara ya TANESCO, Spika Mbili, vitenge doti Nne, Kopyuta tatu, Subwoofer Nne, Monita moja, Godoro moja, panga moja, shoka moja, makabati mawili ya kuhifadhia Chips, huku wakiokota Pikipiki Nane na Baiskeli 11.
“Tunawaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wafike katika kituo kikubwa cha Polisi Shinyanga mjini kwa ajili ya kuzitambua mali zao kuanzia tarehe 22 hadi 30 mwezi huu,”amesema Magomi.
Aidha, amesema katika kipindi hicho wamefanikiwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani na kutolewa hukumu mbalimbali, wakiwamo wabakaji kuchapwa viboko na kufungwa Jela wakiwamo na watu waliojihusisha na vitendo vya ulawiti, kujeruhi, wizi wa mtoto na kumpa mimba mwanafunzi.
Ametaja kesi zingine zilizotolewa hukumu kuwa ni kupatikana na madawa ya kulevya ikiwamo bangi na Mirugi ambapo wahusika wamefungwa Jela.
Katika hatua nyingine Kamanda, ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za nchi naza usalama barabarani wala kutojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa namna yoyote ile hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Christimas na mwaka mpya ikiwa Jeshi limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo hivyo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari juu ya msako ambao wameufanya ndani ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha vifaa mbalimbali vya wizi ambavyo wamevikamata.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha vifaa mbalimbali vya wizi ambavyo wamevikamata.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesh Bunduki aina ya Gobore ambayo wameikamata katika msako.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha Pikipiki za wizi.
Muonekano wa vitu vilivyoibiwa.
Pikipiki zilizoibiwa.
Baiskeli na vifaa vya TANESCO vilivyoibiwa.