BIBI AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SHINYANGA ATOLEWA UBONGO


Bibi aliyefahamika kwa jina la Mbalu Shija (68) mkazi wa kijiji cha Mwalukwa wilayani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na ubongo kutoka nje akidaiwa ni mshirikina.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7 usiku akiwa amelala nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa kijiji Mwalukwa Lucas Buchambi akisimulia tukio hilo leo, amesema Bibi huyo hua ana kaa na wajukuu zake, lakini usiku huo hawakuwepo walikuwa kwa jirani wakijiandaa maandalizi ya kuimba kwaya kwenye mkesha wa siku sikuu ya Christimas.

Amesema wajukuu zake waliporudi nyumbani usiku huo, ambapo mmoja hua analala na bibi yake alipoingia chumbani akamuona bibi yao ameanguka chini akiwa ameuawa, ndipo akapiga kelele kuomba msaada.

"Baada ya kupata taarifa za tukio hili majira ya saa 8 usiku niliamka nikaenda eneo la tukio na kumkuta bibi huyu akiwa ameuawa vibaya kwa kukatwa mapanga kichwani huku ubongo ukiwa nje," amesema Buchambi.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464