Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyotokea barabara kuu ya Morogoro- Iringa eneo la Iyovi (Mikumi) Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro baada ya gari dogo Toyota Allion IT lililokuwa likitokea Bandarini Dar-es-salaam kuelekea mpakani Tunduma kugongana uso kwa uso na lori la mafuta likitokea Iringa kuelekea Morogoro .
RPC wa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu amesema waliofariki katika ajali hiyo ni Watu watano wakiwemo Wanaume wanne na Mwanamke mmoja ambao walikuwa katika gari la IT.
Kamanda Musilimu amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa wa gari ndogo aliyefahamika kwa jina la Festo Shoo ambaye alitaka kuyapita magari madogo yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari hata hivyo naye alifariki katika ajali hiyo, miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito Mikumi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464