NTIBAZONKIZA,BOCCO WAPIGA HAT TRICK, SIMBA IKIIFUMUA TANZANIA PRISONS 7-1
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba Sc imefanikiwa kuichakaza timu ya Tanzania Prisons kwa kuichapa mabao 7-1, mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake kwa mashabiki wa timu ya Simba kwani walitoka kwa furaha na shangwe haswa baada ya mchezaji wao mpya Said Ntibazokiza kufanikiwa kuanza kwenye mchezo huo na kufanikiwa kupachika mabao matatu (Hat Trick) na kutengeneza goli moja.
Mabao mengine matatu yamefungwa na mshambuliaji wao John Bocco na kufikisha mabao tisa kwenye ligi ya NBC huku akibakiza bao moja kumfikia nyota mwenzake Moses Phiri ambaye yupo nje kwasababu ya majeruhi yanayomsumbua.
Bao la saba la Simba sc limefungwa na beki wao Shomari Kapombe akipokea krosi nzuri kutoka kwa Gadiel Michael ambaye aliingia dakika za lala salama kwenye mchezo huo ambao umekuwa ni kivutio kwa mashabiki
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464