Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDCs.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amewataka wanawake wasinyamaze kimya pale wanapokuwa wakiombwa rushwa ya ngono, na kuwataka wapaze sauti ili wahusika wachukuliwe hatua na kukomesha rushwa hiyo ambayo imekuwa ikiwanyima haki zao.
Magomi amebainisha hayo leo, wakati akizindua Kampeni ya kupinga rushwa ya ngono katika uwanja wa michezo wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga, iliyoratibiwa na Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO), kwa kushirikiana na Takukuru pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC.
Amesema rushwa ya ngono inapaswa kupingwa na kila mtu, ikiwa inarudisha nyuma maendeleo pamoja na Taifa kupata wataalam wasio na sifa sababu ya kutoa rushwa ya ngono, na kuachwa wale waliostahili kupata nafasi hiyo.
“Rushwa ya ngono ni unyanyasaji na kunyamazia kimya rushwa ya ngono ni kunyima haki, kila mtu anapaswa aguswe na hili tatizo na kulipazia sauti hasa wanawake ambao ndiyo waathirika wakubwa wa hii rushwa, msikae kimya toeni taarifa na taarifa hizi zitakuwa za siri,”amesema Magomi.
Naye Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja, amesema rushwa ya ngono siyo fursa ya kujinufaisha, na kuwataka wanawake wafike kwa wingi kwenye taasisi hiyo kutoa taarifa, ili kumkamata mhusika na kumchukulia hatua kali na liwe fundisho kwa watu wengine na hatimaye kuikomesha kabisa.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa, amesema wameendesha Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono kwenye vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), na wameamua kuisambaza elimu hiyo kwa wananchi kwa kutumia mchezo wa mbio za baiskeli na vyombo vya habari.
“Tupo hapa kwa ajili ya kupinga rushwa ya ngono, KTO tunaamini kuwa silaha kubwa ya kupinga rushwa ya ngono ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya rushwa ya ngono ndiyo maana hapa leo tunashuhudia mbio za baiskeli. Tunajenga uelewa kupitia michezo Waendesha baiskeli watakuwa mabalozi wa kueneza elimu ya madhara ya rushwa ya ngono, naomba kila mmoja apinge rushwa ya ngono kwani jambo hili linamhusu kila mwananchi”,amesema Mjengwa.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Maria Mkanwa amesema chuo hicho pamoja na vyuo vingine vya maendeleo ya wananchi kwa kushirikiana na KTO wanaendelea kutoa elimu ya kupinga rushwa ya ngono pamoja na kutoa Proramu mbalimbali kwa ajili ya kumwendeleza mwanamke kijana.
Aidha kauli mbiu ya Kampeni hiyo ya rushwa ya ngono inasema KUWA JASIRI KATAA RUSHWA YA NGONO.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwakilishi wa Bodi ya KTO, Khalfani Mshana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mtoa huduma za kisheria ngazi ya jamii, Anne Deus kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria Community Edivication Organization (CEO) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Maria Mkanwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi C wakishindana mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi C wakishindana mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakijiandaa kuanza mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakichuana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakichuana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwendesha Baiskeli maarufu Makirikiri akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza kundi la wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi B wakitimua vumbi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwendesha Baiskeli Paul Maiga akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza kundi B la Wanaume wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Wanafunzi wa Chuo cha Buhangija FDC wakitoa burudani ya Igizo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Wanawake waendesha baiskeli bila ndoo kichwani wakitimua vumbi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwendesha Baiskeli maarufu Futi Mbili akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Vijana wa kundi la Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakihitimisha mbio baada ya kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 35 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs. Kulia ni Mshindi wa kwanza George Izengo
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya shilingi 50,000/= Mwendesha Baiskeli Makirikiri baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za baiskeli huku umebeba ndoo ya maji kichwani kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 15
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya shilingi 50,000/= Mwendesha Baiskeli Futi Mbili baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za wanawake kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 15
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464