Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga ambaye anasisitiza suala la chanjo ya polio katika wilaya yake.
Na Kareny Masasy, Kahama
MKUU wa
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amesema watumike mabalozi wa nyumba kumi kwenye mitaa,vitongoji na
vijiji katika zoezi la utoaji chanjo ya kinga ya polio kwa watoto chini ya umri wa
miaka mitano.
Kiswaga amesema hayo leo tarehe 1/12/2022 kwenye kikao kazi cha kujadiliana utoaji wa chanjo ya kinga ya Polio kwa awamu zilizopita na awamu ya nne.
Kikao hicho kilikutanisha wataalamu kutoka idara ya afya,lishe na maendeleo ya
jamii wanaosimamia zoezi la chanjo katika halmashauri za Ushetu,Msalala na
manispaa ya Kahama.
Kiswaga
amesema wilaya ya Kahama inachukua nusu ya mkoa wa Shinyanga imepata idadi ya
chanjo 304,600 ambazo zitatoa
kuanzia leo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano nakusisitiza mafaniko zaidi.
“Sipendi
mlegee kwenye tukio hili muendelee kuonyesha mfano…. Kama mlivyofanya utoaji wa
chanjo kwa awamu zilizopita”amesema Kiswaga.
Mratibu wa
chanjo kutoka halmashauri ya Ushetu Ramadhani
Kabuhu akisoma taarifa kwa niaba ya halmashauri zote amesema zoezi la utoaji chanjo litaanza tarehe 1 hadi
4 Desemba/2022.
Maandalizi
ya utoaji chanjo awamu ya nne kwa halmashauri za Msalala,Ushetu na Kahama yamekamilika wanatarajia kuwafikia watoto chini ya umri wa miaka mitano (walengwa)
284,495 na chanjo ya polio iliyopokelewa ni 304,600.
Kabuhu amesema
halmashauri ya Ushetu wamepokea chanjo 98600,Msalala chanjo 107,000 na Manispaa
Kahama chanjo 99,000.
"Kuna timu ya wataalam 549 na maboresho yaliyofanyika kuongezwa kwa timu ya watu 20 ya utoaji chanjo kwa kila halmashauri kuweza kuwafikia watoto wote"amesema Kabuhu.
Wataalamu wote wamekiri mbele ya mkuu wa wilaya maandalizi yako vizuri wataalamu wamejiandaa kufanya zoezi hilo kwa kuwafikia watoto kila kona pamoja na kuwafuata shambani.
Hata hivyo mkoa wa Shinyanga unatarajia kutoa chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano 521,025 na kupokea dozi ya chanjo 614,800 ikiwa wataalamu 1,021.
Wizara ya
afya kwa kushirikiana na wadau wa sekta
ya afya imeendelea kuchukua hatua
mbalimbali za kukabiliana na tishio la mlipuko wa ugonjwa wa polio hapa nchini.
Ugonjwa wa
polio ni ugonjwa unaosababishwa na
kirusi ambacho huambukizwa kutoka kwa
mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine kwa kula au kunywa kitu kilichochafuliwa na
kinyesi chenye virusi vya polio.
vinapoingia katika mwilini huathiri
mfumo wa fahamu na kusababisha
madhara ya kiafya ikiwemo kupooza
kwa ghafla viungo vya mwili.