KANISA LA PHILADELFIA MIRACLE TEMPLE SHINYANGA LIMETOA MSAADA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NDEMBEZI


Mchungaji wa kanisa la Philadelfia Miracle Tample Baraka Laizer akitoa sadaka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi

Suzy Luhende,Shinyanga Blog


Kanisa la Philadelfia Miracle Temple lililopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga limetoa msaada kwa watoto 21 wanaoishi katika mazingira magumu katika mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga.

Msaada huo umekabidhiwa leo na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Baraka Laizer kwa watoto hao, ambapo ameahidi kwamba kanisa litaendelea kuwasaidia watoto hao mpaka watakapo kuwa watu wazima.

Laizer ambaye amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana na waumini wa kanisa amesema lake,  kwa niaba ya kanisa la Philadelfia Miracle Tample ametoa vitu vyenye thamani ya shilingi zaidi ya laki 300,000, pia anapenda kuwasaidia watoto hao ili wajisikie vizuri kama watoto wengine wanaoishi kwenye familia zenye uwezo.

"Leo nimeamua kuja kula pamoja na watoto hawa chakula cha mchana ili kudhihilisha upendo pamoja na kuwapa hiki kidogo kilichotolewa na Kanisa la Philadelfia Miracle Temple, ambacho ni Sukari na Sabuni za kufulia nguo za shule zitawasaidia na tutaendelea kuwasaidia kwa jinsi tutakavyojaaliwa na mwenyezi Mungu,"amesema Laizer.

Laizer amesema watoto wengi waliopo hapa ni wale walioachiwa kina bibi wanawalea, hivyo kanisa litashirikiana na kinabibi hao katika kuwalea watoto hao, lakini pia ameahidi kwamba kabla ya kufungua shule kanisa litawanunulia daftari na kalamu ili waweze kusoma vizuri nakutimiza ndoto zao.

"Tunawakaribisha sana wadau mbalimbali wanaoguswa kusaidia watoto hawa waungane nasi katika kushiriki baraka za bwana, kwani watoto hawa wanahitaji kupata magodoro vitanda na vitu vingine vya kuwasaidia ili waweze kujisikia vizuri,amesema Laizer.

Mama mchungaji wa kanisa hilo Evaline Msangi amesema walichokifanya leo ni mwanzo tu, hivyo kanisa litaendelea kuwasaidia watoto hao zaidi nazaidi na kuhakikisha wanakuwa watu wazima na kujitegemea.

Baadhi ya wazazi wenye watoto hao Janeth Limbu na Monica James wameshukuru kwa msaada huo, wameliomba kanisa liendelee na moyo wa upendo, hivyo waendelee kuwakumbuka pamoja na wadau wengine waungane na kanisa hilo kuweza kuwasaidia kwa chochote watakachojaaliwa watashukuru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa Onesmo Mahenda amemshukuru mchungaji na kanisa zima kwa kujitoa kwao, kwani toka achaguliwe kuwa mwenyekiti hajawahi kuona kanisa likitoa msaadawa aina yoyote kwa wahitaji wa mtaa wake,hivyo ameona ni mjiza mkubwa kukumbukwa watu wake.

Hata hivyo mchungaji baraka aliambatana na baadhi ya wazee wa kanisa, mwenyekiti wa wanawake na baadhi ya waumini wa kanisa hilo kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.




Mchungaji wa kanisa la Philadelfia Miracle Tample Baraka Laizer akitoa sadaka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi


Mchungaji Baraka akiendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Watoto baada ya kupewa zawadi yao

Mchungaji baraka akipongezana na mjumbe wa mtaa huo Anania Clementi ambaye pia ni mchungaji wakanisa la Philadelfia Miracle Temple




Mchungaji Baraka akiendelea kutoa zawadi hizo kwa wahitaji

Mchungaji Baraka akikabidhi sadaka kwa mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa Onesmo Mahenda


Mchungaji Baraka akiendelea kugawa sadaka kwa watoto






Watoto na baadhi yawazazi wao wakisubiri kupewa zawadi zao walizoandaliwa na kanisa la Philadelfia Miracle Temple

Watoto na baadhi ya wazazi wakila chakula cha pamoja kilichoandaliwa na kanisa la Philadalfia Miracle Temple


Mchungaji Baraka akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto ambao ataendelea kuwasaidia









Mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa akifafanua jambo kwa mchungaji Baraka


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464