KIWOHEDE YAWATAKA WASICHANA KUZIDI KUJITAMBUA KUEPUKA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.



Mkurugenzi wa shirika la KIWOHEDE  Justa Mwaituka akicheza na  wahitimu wa  chuo cha ufundi Stadi  kilichopo Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Na  Kareny  Masasy, Kahama

WAHANGA wa mimba na ndoa za utotoni 124  wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali kutoka  chuo cha ufundi stadi (Veta)  cha ST  Francis de Sales Technical Institute  kilichopo Mwakata  wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Wahitimu hao wametakiwa   kujiunga vikundi  ili kupata mkopo  kwenye halmashauri zinazotengwa za asilimia 10 kwa wanawake,vijana na walemavu.

Mkurugenzi  Justa Mwaituka kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la KIWOHEDE amesema  hayo jana kwenye mahafali ya sita tangu kuanza kuwawezesha wasichana kupitia mradi wa  kufikia usawa wa kijinsia kuwawezesha wanawake na wasichana.

“Wasichana  waliopata mafunzo ni  374  kupitia chuo cha  Mwakata wilayani Kahama  kinachomilikiwa na  kanisa la Roman Katoliki wanaohitimu ni 124 na wanaendelea na masomo ni 250”amesema Mwaituka.

Mwaituka amesema mafunzo wameyasimamia wao nakupata  kozi ya muda mrefu kwa kufadhiliwa na mashirikiano ya shirika la idadi ya watu duniani (UNFPA),UNWOMEN na KOICA.

Mwaituka amesema wasichana hao wametoka katikahalmashauri mbili za Msalala   mkoani Shinyanga wasichana 75  na Ikungi mkoani Singinda  wasichana 49  walipatikana kwa utaratibu kwa kushirikiana na serikali.

“Nafahamu mnahitimu mafunzo yenu mliyoyapata kwa kipindi cha miaka miwili hivyo mmependeza msikubali  kurubunika tena badala kutumia ujuzi mlioupata kujinyanyua kimaisha”amesema  Mwaituka.

“Fani ya muda mrefu  wapo wanafunzi 37 ikiwa fani ya umeme wanafunzi  5,fani ya ushonaji 57,fani ya ufundi wa magari  na udereva 5 uhazili na Tehama 15 fani  ya salun na mapambo 42”amesema  Mwaituka.

Ofisa maendeleo kutoka halmashauri  ya Ikungi Friday Zacharia amesema  wanajitahidi kuwapatia mikopo  wasichana hao  baada ya kuwa wamemaliza ufundi changamoto iliyopo vikundi vyao havidumu vinasambaratika.

Paroko wa parokia  jimbo kuu Tabora Charles Ouma wakati akitoa mahubiri kwa wahitimu hao amesema waichana wamekuwa wakitumika  kwenye biashara za ngono  hivyo wasitumike bali watumie ujuzi wao kujiajiri na kupata kipato.


Wasichana kutoka halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama na Ikungi mkoani Singida wakiingia ukumbini

Wahitimu wakifurahia kwa kucheza

Mkurugenzi wa  shirika la KIWOHEDE  Justa Mwaitusa  akiwa meza kuu na  kaimu ofisa maendeleo wa halmashauri ya  Msalala     Veronica  Msuko.

Viongozi wakiwa meza kuu katika mahafali




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464