Na Shinyanga Press Club Blog
Jamii imetakiwa
kuendelea kuwafichuwa watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana
na kuwa chanzo cha umasikini kwenye familia na kuharibu ndoto za watoto kwa
kuwakatisha masomo kutokana na kupata ujauzito katika umri mdogo pamoja na
kukomesha ndoa za utotoni.
Akizungumza
na wakazi wa Kata ya Nsalala Mkurugenzi wa Shirika la (TVMC)lenye makao makuu
yake Manispaa ya Shinyanga Mussa Ngangala,amesema katika kuadhimisha siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia wameamuwa kuwafikia wananchi vijijini ili kutoa elimu
itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo ambavyo bado ni changamoto kwenye jamii.
Ngangala
amesema kila mtu anawajibu wa kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa
kijinsia na kuhakikisha wanakuwa salama wakati wote wanapokuwa nyumbani na
shuleni,kutokana na vitendo vya ukatili kuisababishia hasara serikali kwa
kutumia fedha nyingi kuhudumia mazura wa ukatili.
Kwa upande
wa mimba na ndoa za utotoni,Mussa ameiomba jamii kuacha kuwalinda watu
wanaoharibu ndoto za watoto wao kwa kuwakatisha masomo baada ya kupata
ujauzito,badala yake wawe mstari wa mbele kutoa taarifa kwa viongozi ili
wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha matukio hayo.
“Bado tuna
changamoto kubwa ya mimba na ndoa za utotoni sasa ni jukumu letu sisi sote kama
wazazi kupinga vitendo hivyo ili viweze kukoma na kuwawezesha watoto kufikia
ndoto zao, hakikisheni mnafuatili mienendo ya watoto wenu wanapokuwa nyumbani
hasa wakati wa likizo pia kujua changamoto wanazokumbana nazo wanapokwenda
shule”amesema Ngangala.
Nao baadhi
ya wakazi wa Kata ya Nsalala Juliana Paul na Kazimili Shuhuli wamesema vitendo
vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni tatizo kubwa na kuiomba
serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kusaidia kukomesha vitendo vya
ukatili kwa watoto na kuchukuwa hatua kali.
Wakazi hao
wa Nsalala wamesikitishwa na kitendo cha
watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwemo wanaowapa mimba
wanafunzi kuachiwa huru na kuonekana mitaani wakitoa maneno ya majigambo jambo
ambalo wamesema linaongeza machungu kwa
mazura wa ukatili kutokana na kukaa muda mfupi na kurejee tena mitaani na
kuiomba serikali kuchukuwa hatua kali za kisheria ili liwefundisho kwa wengine.
Wananchi wa Nsalala
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464