Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizindua rasimi madarasa yaliyojengwa katika shule ya Ngokolo sekondari manispaa ya Shinyanga
Suzy Luhende,Shinyanga Blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakae kwa amani na furaha kwa sababu Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu anaendelea kuwakumbuka kwa kuleta fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo yakiwemo madarasa na maabara.
Suzy Luhende,Shinyanga Blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakae kwa amani na furaha kwa sababu Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu anaendelea kuwakumbuka kwa kuleta fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo yakiwemo madarasa na maabara.
Hayo ameyasema leo baada ya kukagua na kupokea madarasa ya shule ya Ngokolo sekondari iliyopo kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ambapo amesema tangu aingie madarakani Rais Samia Suluhu hajawasahau wananchi wake anaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali.
Mjema amesema amekagua na kuyaona madarasa yamekamilika na yamejengwa kwa kiwango kinachotakiwa, hivyo ameridhika nayo, ambapo katika mkoa wa Shinyanga walipangiwa kukamilisha madarasa 332 ambapo fedha zilizoletwa kwa ajili ya ujenzi huo ni Sh 6.64 Bilioni.
Amesema katika wilaya ya Shinyanga mjini na manispaa walipangiwa kujenga madarasa 61 ambayo gharama yake ni Sh 1.4 bilioni, hivyo ameyakagua na kuridhika nayo kuwa yanakiwango kizuri kinachotakiwa hivyo amewataka wanafunzi wayatunze ili waje watumie na kizazi kingine kijacho.
"Tumeyakagua na kuyaona madawati haya yanakiwango cha kutosha kabisa hivyo tumeridhishwa nayo na tumeyapokea kwa sababu yamekamilika kwa asilimia 100, hivyo watoto wangu someni kwa bidii mfaulu vizuri Rais anawapenda ndiyo maana anaendelea kuleta fedha ili muweze kusoma kwa furaha na amani hii yote ni juhudi ya Rais tuendelee kumuombea ili aendelee kuleta maendeleo zaidi"amesema Mjema.
Aidha amesema mkoa wa Shinyanga ulipangiwa kutengeneza madawati 2440 na yamekamilika 1344 ambayo bado hayajakamilika mpaka sasa ni 1069,wamesema kufikia tarehe 22 mwezi huu yatakuwa yamekamilika kwa asilimia 100 hivyo atayapokea.
"Viongozi mmesema ndani ya wiki mbili mtakuwa mmekamilisha madawati yote kwa asilimia 100 hivyo tarehe 22 nitakuja kuyapokea, hivyo tumepokea madarasa tu kitu ambacho hatujakipokea ni madawati, madawati yamekamilika, umeme upo, mbaabara zipo za kutosha hivyo mshindwe kufaulu ufaulu wa juu tu watoto wangu,"alisema Mjema.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira, amempongeza mkuu wa mkoa kwa kazi kubwa ya kusimamia miradi ya maendekeo yakiwemo madarasa, alisema kazi ya kupokea madarasa ni kielelezo cha kazi kubwa aliyoifanya kwa mkoa mzima.
"Sekta ya Elimu Rais alisisitiza kuwa hakuna Taifa lolote ambalo litafanikiwa bila elimu badala yake tutaendelea kuwa watumwa bila elimu hatuwezi kupata maarifa na ujuzi, hivyo ni vizuri tuzingatie elimu ili taifa letu liweze kuwa na watu wasomi,"amesema Katambi.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Magile Makombe amesema chama cha mapinduzi kinasimamia irani ya chama, hivyo kwa maendeleo yanayoonekana ni irani ya CCM, madarasa yamekamilika hatutegenei kuona upungufu wa madarasa, hivyo ili tuendelee kufanya vizuri tuwaombe wananchi waendelee kutoa ushirikiano wa hali na mali.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Ngokolo George Mwandu amesema kwa kupokelewa kwa madarasa wanashukuru sana ambayo yameonekani ya kiwango hivyo wataendelea kusimamia miradi mbalimbali ili kuhakikisha inakuwa ya kiwango zaidi.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Magile Makombe akizungumza baada ya mkuu wa mkoa kupokea madarasa katika shule ya Ngokolo sekondari
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Ngokolo George Mwandu akizungumza
Viongozi mbalimbali wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wakimsikiliza kwa makini
Viongozi mbalimbali wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema wakimsikiliza kwa makini
Viongozi mbalimbali wa wilaya baada ya kushuhudia kupokelewa kwa madarasa ya shule ya Ngokolo yenye kiwango
Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza baada ya kupokea madarasa yenye kiwango
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira, akizungumza
Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga akizungumza baada ya mkuu wa mkoa kupokea madara
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza kabla ya kupokea madarasa hayo
Viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Ngokolo wakimsikiliza mkuu wa mkoa akizungumza na wananchi wa Ngokolo