WANAWAKE WA KATA YA NYIDA WAHOFIA USALAMA WAO KWA VIPIGO NA WANYAMA PORI KWA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA.
Wanawake wa kata ya Nyida ,Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika foleni ya kusubili kupata maji kwa ajili ya familia zao.Baadhi ya wanawake wa kata ya Nyida ,Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika foleni za kuweza kupata maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao
Mtoto wa kata ya Nyida akichota maji kwa ajili ya matumizi katika kisima cha asili kinachotegemewa na wakazi wa eneo hilo.Kisima cha asili kinachiotegemewa na wanawake na watoto wa kata ya Nyida kwa mahitaji ya familia zao kila siku.
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa kata ya Nyida halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga kutoka kaya 1000 wanakabiliwa na changamoto ya
kukosa huduma ya maji safi na salama hali inayowalazimu kuchangia maji na
wanyama wa kutokana na kutumia visima huku, wakiamka usiku wa manane kuwahi foleni
na kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Wakazi hao wa kata ya Nyida
walipozungumza na Shinyanga Press Club blog ndani ya wiki ya mwisho wa novemba,2022,
walielezea kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama hali inayosababisha
kutumia muda mrefu kukaa kwenye foleni kusubiri maji na kuamka usiku wa manane
huku ndoa zao zikiwa hatarini kuvunjika.
Wanawake wa kata hiyo wamelalamikia
kupoteza muda mrefu katika kupata maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao na
wamejikuta wanaingia katika migogoro na wanaume wao kwa kutuhumiwa kujihusisha
na mapenzi na watu wengine wakati wakiwa katika shughuli za kusubili
upatikanaji wa maji.
Khadija Nkinga ,Alisema wanayo changamoto ya maji kwa muda mrefu na wanaiomba serikali iwasaidie kutatua changamoto hiyo
"serikali itusaidie kwa kuwa tunakutana na fisi wakati wa kufata maji katika visima vya asili "Alisema Khadija.
Rachel Pius alisema kutokana na hali ya ukame kuna wakati wamama wanabeba madumu mengi sana ili kupata maji ya kutosha kwa familia zao.
"Hii inasababisha mama kubeba madumu mengi,mama anaweza kubeba madumu hata 12 kutokana na ukame"Alisema Rachel
Aidha Suzana Maganga,alieza kuwa wanapigwa na wanaume zao wakati mwingine kwa kuhisiwa kuwa katika mambo ya mapenzi kutokana na kuwajikuta wanachota maji hadi usku.
"Kwa haya maji tuanapata changamoto,wanaume zetu wanatupiga,wanasema tunakuwa kwenye mambo zetu,maji siku zingine tunapata usku"Alisema Suzana.
Kwa upande wake,Mtendaji wa kijiji cha kata ya Nyida,Steven Misalaba alisema,kijiji kina changamoto ya majikwa kuwa tunatumia visima vya asili tu.
"Asilimia kubwa ya tunatumia visima vya asili na hata hivyo maji yake bado ni ya chumvi" Alisema Steven.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya nyida,Daud Lazaro alisema hatuna vyanzo vya uhakika vya maji hasa kipindi cha ukame hususani vijiji vyote vitatu,tunategemea visima vifupi ambavyo ni vichache kuweza kumudu msimu wote.
"Tunaendelea kuwasilisha maombi kwa serikali ili kuweza kupatiwa maji ya ziwa viktoria ambayo yako karibu kutoka eneo hili"Alisema Lazaro.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyida Daud Lazaro akizungumza na mwandishi wa shinyanga Press Club blog.Khadija Nkinga mkazi wa kata ya Nyida akizungumzia ukosefu wa maji katika eneo lake
Rachel Pius mkazi wa kata ya nyida akizungmza na shinyanga press club blogSuzana Maganga akizungumza na Shinyanga Press Club
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464