Afisa mradi kutoka shirika la SHDEPHA+ Erick Mlimba akielezea utekelezaji wa mradi wa Uviko-19.
Na
Kareny Masasy,Kahama
WAKAZI 197,982 wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama
mkoani Shinyanga wamepata chanjo ya
Uviko-19 kwa hiari kuanzia mwaka 2021
hadi tarehe 15, mwezi Januari,2023.
John
Maongezi ambaye ni afisa mradi kutoka shirika la AMERICARE lenye makazi yake nchini Marekani ameongea na waandishi wa habari leo tarehe 17/01/20 23 mjini Kahama.
Maongezi
amesema wao wamelifadhili shirika la
SHDEPHA+ lenye makazi yake wilayani Kahama kwaajili ya
kuendeleza kutoa elimu kwenye jamii juu ya Uviko-19 na wamekuwa
wakifanya kazi pamoja na wizara ya afya.
Kwa mkoa wa
Shinyanga tumeanza kazi rasmi mwezi wa kumi mwaka 2022 katika
halmashauri ya Msalala,Kishapu na Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha wanasogea karibu kutoa huduma na kuhamasisha uchomaji wa chanjo.
Katika
juhudi za kukwamua mlipuko wa Uviko-19 serikali ya Tanzania mwaka 2021 ilikubali maekezo ya shirika la afya duniani (WHO) kuhusu uchanjaji
wa chanjo na wadau kuendeleza suala hilo.
“Walengwa
waliotakiwa kuchanjwa ni 164,259 na kila halmashauri ilipewa lengo lake na
Msalala imevuka lengo nakufikia asilimia 102.2”amesema Maongezi.
Ameongeza “Tumefikia
lengo lakini uchanjaji bado unaendelea kwani watu wa kuchanja wanahitajika
sababu wapo wenye umri wa miaka 18 wamefikisha wanahitaji kuchanja”
Maongezi
amesema baadhi ya watu walizungumza kwa kupotosha kuwa ukichanja damu itaganda
hawata zaa, watakuwa mazombi lakini
waliochanja wako vizuri na wajawazito wanazaa na hakuna mtu aliyekuwa zombi
wala kuganda damu” amesema
Afisa Mradi
kutoka SHDEPHA+ Erick Mlimba amesema malengo ya mradi ni kuongeza uchanjaji
wa chanjo katika njia tofauti tofauti ikiwa njia mojawapo kusambaza elimu
sahihi nakufanya majadiliano na watu ambao wamekuwa na wasiwasi kuanzia ngazi
ya vitongoji hadi mkoa pamoja na
Kuunganisha jamii na watoa huduma.
Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Peter
Shimbe ambaye ni muelimishaji wa masuala ya afya anasema Covid-19 bado ipo na watu waendelee kujikinga kwa kuchanja.
Mratibu wa
chanjo halmashauri ya Msalala Basil
Kafunja anasema watu walikuwa na mtazamo hasi nakupotosha kuhusu chanjo ya uviko-19 kwa sasa wameelimika na wamekuwa wakijitokeza kwa hiari kuchanja.
“Serikali imeenda mbali zaidi kwa kutumia
mbinu ya wauguzi kutembea kwenye kila nyumba
kuwafikia walengwa ambapo kuanzia mwezi Juni mwaka 2021 hadi Januari
15,2023 wamefanikiwa kuwachanja watu
197,982 sawa na asilimia 102.2”amesema Kafunja. .
Afisa mradi wa kuhamasisha uchanjaji na watoa huduma kwa jamii Erick Mlimba akiwa na mtathimini na mfatiliaji Elizaberth Laurent. kutoka shirika la SHDEPHA+
Afisa mradi kutoka shirika la Americare John Maongezi
kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Peter Shimbe akiwa na mratibu wa chanji Basil Kafunja wakisikiliza utekelezaji wa mradi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464