BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETI SH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO



Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani la kujadili na kupitisha mpango na bajeti ya mwaka 2023/2024 .

Suzy Luhende,Shinyanga blog

Kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga kimejadili na kupitisha mpango wa bajeti wa mwaka 2023/2024 Jumla ya Shilingi Bilioni 39.4 
ambazo zitatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo.
ambapo bajeti ya Tarura ikiwa ni Shilingi zaidi ya bilioni 4.

Wakijadili ajenda ya kikao maalumu cha baraza la madiwani la kujadili na kupitisha mpango na bajeti ya mwaka 2023/2024 madiwani wa halmashauri hiyo  wamesema bajeti hiyo itatumike kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoainishwa  na kuhakikisha inaondoa changamoto zote za halmashauri zilizopo.

Diwani wa kata ya Seke Bugoro Fednand Mpogomi amesema bajeti hiyo waliyoipitisha wanatakiwa wakaisimamie ipasavyo, pia amempongeza Meneja wa Tarura kwamba anafanya kazi yake kwa kujituma, lakini pia amesema kuna baadhi ya wakandarasi ni mizigo hawafanyi kazi zao kwa kiwango wanatakiwa wachunguzwe wasiendelee kupatiwa kazi.

"Bajeti yetu tumeipitisha leo, tunasisitiza wakuu wa idara na sisi wenyewe madiwani twendeni tukazisimamie  kikamilifu fedha zetu tulizozipitisha wenyewe  kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri yetu na zikatatue changamoto za watu wetu ili kuhakikisha kero zilizopo zinaisha,"amesema Mpogomi.

"Pia naomba barabara ya Wishiteleja kwenda Mipa haimo kwenye bajeti hii naomba ihamishiwe kwenda Tanroad kutoka Tarura kwani ni barabara kubwa inaunganisha barabara ya lami kutoka Mwanza kwenda bariadi kupitia kijiji cha Mwakolongo inakutana na rami ya bariadi, kwa sababu tunaujenzi wa Reli bandari kavu, hivyo mizigo mingi itapitia pale,"ameomba Mpogomi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya ambaye ni diwani wa kata ya Mondo ameagiza bajeti hiyo ikasimamowe na kuheshimiwa, ikafanye kazi inayotakiwa, madiwani wote na watendaji wakashirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa kuzingatia idara yake.

"Bajeti hii imepitishwa kwa makusudi watumishi na madiwani simamieni ipasavyo lengo la serikali ni kuona mapato yanasimamiwa kwa asilimia 100, pia Rais wetu mama Samia Suluhu ametupa fedha nyingi sana  kwa ajili ya miradi  mbalimbali ya maendeleo,hivyo tunaomba asituchoke aendelee kutusaidia tuisimamie na tuhakikishe miradi yetu inakuwa ya kiwango zaidi,amesema Jijimya.

Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu  Shadrack Kengese bajeti hii iliyopitishwa leo ikasimamiwe na miradi ya mkakati iliyopo ikasimamiwe na kukamilishwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani yakafikiwe, ili wilaya ya Kishapu ikawe ya mfano.

Aidha mkurugenzi wa halmashauri hiyo Johnson Emmanuel amesema bajeti hiyo iliyopitishwa wataisimamia ipasavyo ili kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo ya halmashauri ya Kishapu.


Diwani wa kata ya Kiloleli halmashauri ya Kishapu Edward Manyama akimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa halmashauri hiyo akiwataka madiwani wakasimamie bajeti kikamilifu



Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizungumza kwenye kikao cha madiwani



Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza kwenye kikao cha madiwani





Diwani akizungumza kwenye kikao

Diwani wa kata ya Seke bugolo Fednand Mpogomi akizungumza kwenye kikao cha madiwani



Madiwani wa viti maalumu kutoka wilaya ya Kishapu wakisikiliza kwa makini

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti



Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya Mwaka 2023/2024



Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti



Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti



Fednand Mpogomi akisisitiza jambo kwenye kikao hicho
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464