AUWA FAMILIA NZIMA BAADA YA MKEWE KUDAI TALAKA KISHA AKAJIUA KWA KUJIPIGA RISASI



Dar es Salaam. Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 katika Jimbo la Utah nchini Marekani amewapiga risasi watu saba wa familia yake kabla ya kujiua mwenyewe, baada ya mkewe kudai talaka.


Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji za Uingereza (BBC), polisi katika jimbo hilo wamesema familia ya watu wanane ilipatikana wakiwa wamefariki ndani ya nyumba katika Jiji la Enoch Jumatano usiku wakati wa ukaguzi wa ustawi katika maeneo hayo.Polisi wanasema waliouawa ni pamoja na mke wa mwanamume huyo, watoto wake watano na mama mkwe wake.

Meneja wa Jiji Rob Dotson amesema mji huo wenye watu wapatao 8,000 ulikuwa katika mshtuko.


Katika mkutano na wanahabari uliofanyika Alhamisi Januari 5, maofisa wa jiji hilo walisema mfanyabiashara wa bima mwenye umri wa miaka 42, Michael Haight aliwafyatulia risasi mkewe Tausha mwenye umri wa miaka 40, mama mkwe wake Gail Earl mwenye umri wa miaka 78 na watoto wake watano kabla hajajiua.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464