UTHAMINI MALIPO YA FIDIA WAATHIRIKA TOPE LA MGODI ALMASI MWADUI WAFIKIA PATAMU, BWAWA LILILOBOMOKA KINGO LAFANYIWA UKARABATI

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almas Mwadui Bernard Mihayo akizungumza na waathirika wa tope la Mgodi huo juu ya hatua ya uthamini na ulipwaji fidia.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

UTHAMINI wa mali kwa Waathirika wa tope la Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited), wakazi wa vijiji vya Ng’wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu upo katika hatua za mwisho ili walipwe fidia.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, amebainisha hayo leo Januari 11, 2023 wakati wa kikao na Waathirika wa tope la Mgodi huo, kwenye utoaji wa elimu wa fomu namba tatu ya uthamini namna watakavyolipwa fidia kulingana na mali zao zilivyoathirika, kabla ya kwenda fomu namba Nne ambayo itaonyesha fidia watakayolipwa kwa kila mmoja.

Amesema utaratibu wa uthamini wa mali za Waathirika wa tope la Mgodi huo upo katika hatua za mwisho, ambapo kesho wataanza mchakato wa kuonyesha wananchi fidia ambayo watalipwa kila mmoja kwa mujibu wa sheria, na hakuna ambaye ataonewa ili kila mtu apate haki yake na kurudi katika maisha yao ya kawaida.

“Nawaombeni mtakapopata fedha za fidia mzitumie vizuri katika maendeleo, na siyo kwenda kufanya mambo ya Anasa na kurudi kwenye umaskini na wanaume kukimbia familia, tunataka muendelee na maisha yenu kama zamani,”amesema Mihayo.

Naye Mthamini kiongozi Richard Sabini, amesema watu ambao watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria, ni wale ambao ni wamiliki wa nyumba na ardhi na siyo wapangaji, ambao wao watalipwa mali walizopoteza, na kubainisha kuwa katika uthamini wao watalipwa watu 180.

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa, amesema mgodi huo tayari umeshafanya ukarabati wa kingo la bwawa lililobomoka, pamoja na kuweka matuta ili kuzuia tope lisivamie tena makazi ya watu.

Nao baadhi ya Waathirika wa tope hilo wameuomba Mgodi huo uharakishe zoezi hilo la ulipaji fidia, ili kila mtu achukue chake na kutafuta mahali pa kuishi sehemu ambayo wanaitaka na kuendelea na maisha yao, huku wakiushukuru Mgodi kwa kipindi chote tangu Novemba 7 mwaka jana walipopata matatizo, wamekuwa wakiwahudumia huduma zote za kijamii ikiwamo chakula na malazi.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almas Mwadui Bernard Mihayo akizungumza na waathirika wa tope la Mgodi huo juu ya hatua ya uthamini na ulipwaji fidia.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almas Mwadui Bernard Mihayo akizungumza na waathirika wa tope la Mgodi huo juu ya hatua ya uthamini na ulipwaji fidia.

Mthamini kiongozi Richard Sabini, aktoa ufafanuzi namna ya zoezi la uthamini lilivyoendeshwa na hatua za ulipwaji fidia kwenye kikao hicho.

Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui kutoka vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha uthamini wa mwisho wa mali zao ili waanze kulipwa fidia.

Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa akizungumzia namna walivyokarabati maeneo ya kingo ya bwawa la tope sehemu lililopasuka na kuleta athari kwa wananchi.

Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa akionyesha namna walivyokarabati kingo za bwawa la mgodi huo ambalo lilibomoka na kuleta athari kwa wananchi.

Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa akionyesha namna walivyokarabati kingo za bwawa la Mgodi huo ambalo lilibomoka na kuleta athari kwa wananchi.

Muonekano wa kingo namna ilivyokarabatiwa na kuzibwa kabisa ili kusitokee tena madhara ya kutiririsha tope kwenda kwenye makazi ya watu ambao wanaishi jirani na Mgodi huo wa Almasi Mwadui.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464