MAKAMU WA RAIS DKT, MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI MPYA YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango (kulia) akiweka jiwe la Msingi katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameweka jiwe la msingi katika Hospital mpya ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kuahidi Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

Uwekaji wa jiwe hilo la msingi katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga umefanyika leo Januari 18, 2023 kwenye hospitali hiyo na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza mara badaa ya kuweka jiwe la msingi, amesema Serikali imedhamilia kuboresha na kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi, na ndiyo maana Rais Samia ametoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa mkoa wa Shinyanga na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

“Wauguzi na Madaktari endeleeni kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi, na msiwatolee lugha chafu wagonjwa wala kuomba Rushwa, pia katika vituo vya afya mtenge madirisha ya wazee na kuwahudumia vizuri,”amesema Makamu wa Rais Dkt Mpango.

Katika hatua nyingine amesema Rais Samia ametoa fedha Sh.bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilomita 5.2 kufika kwenye Hospitali hiyo na kuiondoa barabara ya vumbi iliyopo, na Sh.bilioni 6 kujenga majengo ya maabara na huduma za mama na mtoto.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Moleli, amesema Serikali katika Mkoa huo wa Shinyanga imetoa kiasi cha fedha Sh, bilioni 19.5 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya mkoani humo, pamoja na kununua vifaa tiba ikiwamo CT-SCAN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango  akiweka jiwe la Msingi katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango akiangalia vifaa tiba katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akiwa na viongozi mbalimbali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango akiangalia vifaa tiba katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akiwa na viongozi mbalimbali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango akiangalia vifaa tiba katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akiwa na viongozi mbalimbali.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464