MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI WA ZIWA VICTORIA TINDE, AKERWA WAWEKEZAJI WAKUBWA KUIBA MAJI

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango (wapili kulia) akiweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ameweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde wilayani Shinyanga, maji ambayo yanapelekwa pia katika Mji wa Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.

Dkt, Mpango ameweka jiwe hilo la Msingi leo Januari 19, 2023 katika Tangi la Maji lililopo Buchama Kata ya Tinde wilayani Shinyanga, mradi wa maji ambao utahudumia vijiji 22 vya Tinde na kunufaisha wananchi Elfu 60.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuweka jiwe hilo la Msingi, amesema utekelezaji wa miradi ya maji ipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 97, na kuahidi Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi sababu maji ni muhimu kwa uhai wa binadamu na wanyama.

Amesema Tangu mwaka 2015 hadi 2019 Jumla ya Miradi ya Maji ambayo Serikali imeitekeleza ni 1,423, vijijini 1,268 na Mijini 155, na kuwataka wananchi waitunze miundombinu ya miradi hiyo, pamoja na vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kulinda uoto wa asili.

“Sekta ya Maji ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa viwanda na kupambana na umaskini, na katika mradi huu wa maji wa Tinde utakuwa na faida kwa wananchi na kuwaepusha kupoteza muda mrefu wa kufuata maji safi salama, pamoja na kutopata magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu,”amesema Dk, Mpango.

Katika hatua nyingine Dk, Mpango ameviagiza vyombo vya dola, pamoja na Kamati za ulinzi na usalama kuwasaka wale wote ambao wamekuwa wakijihusisha na wizi wa maji wakiwamo wawekezaji wakubwa na kuwachukulia hatua kali ikiwamo kuwatoza faini.

“Wawekezaji wakubwa waache kuiba maji, bali wachimbe visima vya maji na siyo kutuibia maji, na wale ambao wanachepusha maji kwenye mito tena hawana vibali wabomoe vizuizi walivyojenga Wizara ya Maji na Bonde mlishughulikie hili,”ameongeza Dkt Mpango.

Dkt. Mpango pia ameagiza Wakaguzi pamoja na Baraza la uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabwawa yote ya taka sumu migodini ili kusijetokea tatizo kama lilivyotokea katika bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.

Amemwagiza pia Mthamini Mkuu wa Serikali kukamilisha uthamini haraka juu wa waathirika wa Tope wa bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui ,ili walipwe fidia zao haraka na kuendelea na maisha yao.

Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi na kubainisha kuwa katika Mkoa wa Shinyanga kuna miradi ya maji 18 ya kimkakati ambayo inatekelezwa, na wilaya ya Shinyanga kuna miradi mitatu yenye thamani ya Sh.bilioni 1.9.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akisoma taarifa ya Mradi huo wa Maji ya Ziwa Victoria, amesema katika mji huo wa Tinde vitahudumiwa vijiji 22 na kunufaisha wananchi elfu 60, ambapo pia maji hayo yanahudumia na wananchi wa Shelui wilayani Iramba mkoani Singida na ungharama ya Sh.bilioni 24.4.

Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, amepongeza utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa maji jimboni kwake , na kueleza kuwa katika jimbo hilo lina vijiji 126 na mpaka sasa kutakuwa na vijiji 89 ambavyo vinapata huduma ya maji safi na salama, na kusalia vijiji 37 ambavyo navyo vipo kwenye mchakato wa kupata maji.

 Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango (wapili kulia) akiweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde wilayani Shinyanga,

 Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango akipanda mti mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akipanda mti kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akipanda mti kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Tangi la kuhifadhia maji katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi  Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde.

 Hafla ya uwekaji jiwe la msingi ukiendelea wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

 Viongozi na Wabunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya  uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

 Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria  wa Tinde wilayani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali na wananchi wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria Tinde wilayani Shinyanga ikiendelea.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipowasili kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Lucy Mayenga, alipowasili kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Solwa Ahmed Salum, alipowasili kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, alipowasili kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana  na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munisy alipowasili kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) na Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Lucy Mayenga wakisubili kumpokea Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum (kushoto) akiwa na Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Shinyanga Santiel Kirumba (katikati) na Chrtistina Mzava (kushoto)wakisubili kumpokea Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

 Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwenye Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum kwenye Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (katikati) akiteta jambo Mkurugenzi wa (SHUWASA) kulia Mhandisi Yusuph Katopola (kushoto) ni Meneja wa (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela kwenye Hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria wa Tinde wilayani Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464