Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, (kushoto), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni wakizungumza kwneye kikao cha wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WALIMU wa Shule ya Msingi na Sekondari mkoani Shinyanga, wameonya kula Mahindi ya shule (kufanya mapenzi na wanafunzi), badala yake waimalishe ulinzi wa wanafunzi pamoja na kuwafundisha na kupata ufaulu mkubwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Linno Mwageni, amebainisha hayo leo Janauri 20,2023 kwenye kikao kazi cha wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga.
Amesema walimu wanapaswa kuwa walinzi wa watoto, na siyo kujihusisha nao kimapenzi, ili kuwa marafiki zao na kufanya vizuri kitaaluma.
Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, alikazia suala hilo na kuwambia walimu wakitaka Kada ya Ualimu iwashinde ni kula Mahindi ya Shule.
“Ukitaka Kada ya Ualimu ikushinde kula Mahindi ya Shule,”amesema Nchambi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi OR-TAMISEMI, Suzana Nussu akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI),anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde, amewaonya pia walimu kufanya mapenzi na wanafunzi, huku akiwataka pia kuwa marafiki na wanafunzi ili kubaini changamoto zinazowakabili kwani dunia imebadilika na watoto wanafanyiwa sana vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwamo kulawitiwa.
"Wale wenye shule za bweni imarisheni ulinzi mabwenini, watoto wanalawitianam kuna shule mmoja kilanja mkuu alikuwa akilawiti watoto, baada ya yule Mwanafunzi kwenda kushitaki kwa Mwalimu akamwambia mwenzako yupo kidato cha Nne unataka afukuzwe asifanye mtihani, hebu sisi kama wasimamizi wa elimu tulisimamie hili na kuchukua hatua kali,” amesema Nussu.
Aidha, amesema lengo la kikao hicho ni kujenga uelewa wa pamoja na matarajio ya (TAMISEMI) baada ya kikao hicho ni kuona Walimu wanabadili utendaji wao wa kazi na kuacha kufundisha kimazoea.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mosses Chilla akizungumza kwenye kikao hicho kwa Niaba ya Waziri wa (TAMISEMI), Angellah Kairuki, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo elimu bure, kujenga shule,madarasa mapya hali inayosababisha idadi ya wanafunzi kuongezeka shuleni.
“Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu na tunafarijika kuona mafanikio makubwa katika ufaulu wa wanafunzi, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji”,amesema Chilla.
Aidha amewataka wasimamizi wa elimu kuhakikisha wanadhibiti mdondoko wa wanafunzi shuleni inayosababishwa na wanafunzi kutopata chakula, utoro na mambo mengine.
“OR TAMISEMI inaekeleza kila kiongozi wa elimu afuatilie ujifunzaji na ufundishaji ili kuongeza ufaulu. Kila mwalimu na kiongozi yeyote ahakikishe wanafunzi wanapata chakula shuleni”,amesema Chilla.
“Pia ni lazima kuwe na ulinzi wa watoto shuleni, tuwasimamie watoto wetu kwani wanapata matatizo kwa sababu ya kukosa ulinzi. Lakini tufundishe nidhamu kwa wanafunzi,wanafunzi waongee lugha zenye staha na tusisahau kuwafundisha uzalendo wa kitaifa,tuwafundishe kuhusu tunu za taifa”,ameongeza Chilla.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako amezitaja baadhi ya changamoto zinazokabili sekta ya elimu mkoani Shinyanga, kuwa wanafunzi kutembea umbali mrefu, upungufu wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi.
Akizungumzia suala la uandikishaji wanafunzi kwa mwaka huu 2023, amesema hadi kufikia Januari 18 kwa wanafunzi wa shule za msingi wameandikisha wanafunzi asilimia 88, awali asilimia 85, Sekondari kidato cha kwanza asilimia 47.
Kwa upande wa ufaulu kidato cha Nne kuanzia mwaka 2019-2021, amesema mwaka 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 81, 2020 asilimia 84, 2021 asilimia 88, na 2022 matoke bado hayajatoka.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi OR-TAMISEMI, Suzana Nussu akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Moses Chilla akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni akizungumza kwenye kikao hicho.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.
Wasimamizi wa elimu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao.