Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha baadhi ya Nyara za Serikali ambazo zimeibiwa.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limekamata vitu mbalimbali za wizi zikiwamo na Nyara za Serikali, Madawa ya kulevya, na watu 10 ambao walikuwa wakijihusisha na wizi wa mafuta katika ujenzi wa Reli ya kisasa SGR.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, ametoa taarifa hiyo leo Januari 23, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari.
Amesema Jeshi hilo katika msako na doria ambao wameufanya ndani ya mwezi mmoja, wamekamata vitu mbalimbali vya wizi zikiwamo nyaraka za Serikali, ambazo ni mikia 21 ya nyumbu, maganda matano ya mayai ya mbuni, ngozi moja ya paka pori, kipande kimoja cha mbuzi mawe, miba 44 ya nungunungu, vipande vitatu vya mkonga wa Tembo, jino la Tembo, mikia mitatu ya ngiri.
Nyara zingine ni vipande vitatu vya Magamba ya Kobe, kucha tano za Paka Pori, ngozi ya Fungo na Pembe moja ya Korongo.
Aidha, ametaja mali zingine za wizi ambazo wamekamata kuwa ni Mita moja ya Tanesco, Solar moja Tv 4, sabufa moja, mafuta ya Petroli 225, Seti moja ya muziki, Pombe kali aina ya Moshi, Kopyuta moja miundombinu ya mawasiliano ya TTCL na Barabara na madumu 42 yaliyotumika katika wizi wa mafuta.
“Katika msako huu tumekata pia watu 10 ambao walikuwa wakijihusiha na uhalifu katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa SGR , tumekama na mipira ambayo ilikuwa ikitumika kunyonya mafuta na Pikipiki zilizokuwa zikitumia katika wizi huo,” amesema Magomi.
“Pia tumekamata madawa ya kulevya Kete 278 na Bangi kilo 10, na katika kesi mbalimbali watuhumiwa wamefungwa jela ikiwamo kesi ya ukabaji, na ukatili wa watoto,”ameongeza.
Kamanda ametoa pia wito kwa wananchi kuacha kufanya vitendo vya uhalifu, na kuwaomba washirikiane na Jeshi hilo katika kutokomeza uhalifu na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha baadhi ya Nyara za Serikali ambazo zimeibiwa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga akionyesha madumu ambayo yamekuwa wakitumia katika wizi wa mafuta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha Pikipiki ambazo zimekuwa zikitumia katika wizi wa vitu mbalimbali.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha miumbombinu ambayo imeibwa ikiwamo zikiwamo alama za usalama Barabarani na miundombinu ya TTCL.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha zana ambazo zimekuwa zikitumia kupiga Ramlichonganishi.