MADIWANI SHINYANGA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 SH. BILIONI 36.8, UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI WAHIMIZWA



Baraza maalum la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti mwaka wa fedha 2023/2024.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha (2023/2024) kiasi cha fedha Sh.bilioni 36.8.

Wamepitisha mapendekezo ya bajeti hiyo leo januari 24, 2023 kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, huku wakisisitiza kasi ya ukusanyaji mapato iendelee pamoja na kubuni vyanzo vipya ikiwamo ukusanyaji wa ushuru katika madini ujenzi.

Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mensaria Mrema awali akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango huo wa bajeti wa mwaka wa fedha (2023/2024) amesema Manispaa hiyo wanatarajia kukusanya kiasi cha fedha Sh.bilioni 36.8 .

“Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha (2023/2024) tunarajia kukusanya na kutumia Sh.bilioni 36.8 kwa mchanganuo ufuatao, vyanzo ya mapato ya ndani Sh.bilioni 6, Ruzuku ya matumizi mengineyo Sh Milioni 738.6, Ruzuku ya mishahara Sh.bilioni 21,0” amesema na kuongeza

“Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu Sh.bilioni 4.1 na Ruzuku ya miradi ya maendeleo wahisani Sh.bilioni 4.9.”

Nao Madiwani wakichangia mapendekezo hayo ya mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha (2023/2024) akiwamo Juma Nkwabi wa Mwawaza wamesema wamepitisha bajeti hiyo huku wakishauri kasi iendelee kuongezeka ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwamo na ukusanyaji wa ushuru katika madini ujenzi.

Naye Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka, amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kujituma kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani, na hata kuongoza nchini nzima katika ukusanyaji wa mapato mwaka wa fedha uliopita, huku akiwaonya wasibetweke na sifa hizo bali waendelee na kasi hiyo hiyo ya ukusanyaji mapato na kuongeza tena.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewasihi watumishi ambao wanakusanya mapato waendelee kuwa na nidhamu ya fedha, pamoja na kutumia lugha nzuri wakati wa ukusanyaji mapato na kuhifadhi kanzi data, ili kubaini wafanyabiashara ambao wameshalipa mapato na kuondoa kero ya kuwafungia vibanda vyao na wakati walishalipa mapato.

“Bajeti ya mwaka wa fedha (2023/2024) tunakwenda kufanya vizuri zaidi, ila wale ambao mnahusika kwenye ukusanyaji wa mapato, tumieni lugha za weledi sababu watu hawa tunawahitaji ili walipe mapato, na fedha hizo ziendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi,”amesema Masumbuko.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, amesema wataendelea kusimamia nidhamu kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani, pamoja na kufuatilia vyanzo vipya ikiwamo madini hayo ujenzi.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Mensaria Mrema akiwasilisha taarifa ya mapendekezo ya mpango wa Bajeti wa mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye Baraza la Madiwani.

Diwani wa Kizumbi Lubeni Kitinya akichangia kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili mapendekezo ya mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Diwani wa Mwawaza Juma Nkwabi akichangia kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili mapendekezo ya mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto) akiwa na Naibu Meya Ester Makune kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Vitimaalumu Zuhura Waziri akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Ibadakuli Msabila Malale akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Mwawaza Juma Nkwabi akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Vitimaalum Shela Mshandete akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka akiwa kwenye kikao cha Baraza la kupitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti katika mwaka wa fedha 2023/ 2024.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464