HAYA HAPA MAAMUZI YA TFF KWA FEI TOTO

TFF imesema Feisal ni mali ya Yanga
 
 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo January 7 2023 imetangaza maamuzi kuhusu kesi ya Mchezaji Feisal Salum na kusema kuwa Mchezaji huyo bado ni Mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba.

Taarifa ya Kamati hiyo imesema “Kamati imeamua kuwa Feisal bado ni Mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba, uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu January 9 2023, Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya Kamati hiyo ikipinga hatua ya Mchezaji wao kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha”

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko havo iana ambapo pande zote (Yanga na Feisal).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464