Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo akitoa maelezo kwa meneja wa Ruwasa wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emael Nkopi na mtekelezaji wa mradi kutoka kampuni ya Healem Elias Slyvester eneo la mradi wa maji.
Na Kareny Masasy,Shinyanga
MKURUGENZI mkuu wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) Mhandis Clement Kivegalo amefurahishwa na jumuiya za chombo cha watumiaji maji (CBWSO) mkoani Shinyanga kwa ukusanyaji wa mapato na kufanyiwa ukaguzi.
Mhandis Kivegalo ameyasema hayo leo tarehe 14/1/2023 alipohitimisha ziara yake mkoani hapa ya ukaguaji wa miradi pamoja nakukutana na jumuiya za vijiji vya Ng’washi kata ya Pandagishiza na kijiji cha Songambele kata ya Salawe..
Mhandis
Kivegalo amesema jumuiya za watumia maji
zimeanza kupata uelewa tofauti na zamani
ambapo serikali ndiyo inavyotaka wajitegemee.
Mhandis Kivegalo amesema amefurahishwa na jumuiya
za watumiaji maji kijiji cha Songambele wilaya
ya Shinyanga kila mwezi makusanyo zaidi ya
Millioni 19 na jumuiya ya Pasamwash ya kijiji cha Songambele sh Millioni 4.
“Jumuiya
hizi wanapokabidhiwa wanatakiwa kuhakikisha
wanatengeneza vituo vya kutolea maji
pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ”amesema
Kivegalo.
Meneja
wa Ruwasa wilaya ya Shinyanga Mhandis Emael Nkopi amesema miradi inayoendelea mojawapo ni wa kijiji cha
Mawemilu uliopo kata ya Mwakitolyo umekamilika
kwa asilimia 95 gharama yake sh Billioni
3 utanufaisha wakazi 23,000.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya chombo cha watumia maji
kijiji cha Songambele Monica Francis
amesema mradi huo umewanufaisha wananchi nakupata kujiunga kwa wingi baada ya
kuhamasishwa .
Mtendaji wa
jumuiya hiyo Chagu Manyiluzi akisoma taarifa mbele ya mkurugenzi huyo amesema mradi unahudumia
vijiji 10 kwa watu 45,116 chanzo chake
ni bomba la maji ziwa victori
Diwani wa
kata ya Salawe Joseph Buyugu amesema wananchi wanapata huduma ya maji mita 200 kwani walikuwa wakifuata umbali wa kilomita
20 nakufikia hatua ya kubakwa.
Tanki la maji lililojengwa kijiji cha Mawemilu kata ya Mwakitolyo
Mkandarsi wa kampuni ya Halem Elias Slyvester anayetekeleza mardi wa maji kijiji cha Mawemilu kata ya Mwakitolyo akizungumza na mkurugenzi mkuu wa Ruwasa Mhandisi Kivegalo
Ukaguzi wa tanki la maji ukiendelea ambao mradi umekamilika kwa asilimia 95
Watumishi wa Ruwasa wakifuatilia taarifa ya jumuiya ya chombo cha watumia maji kijiji cha Songamele
Mwenyekiti wa jumuiya ya chombo cha watumiaji maji Monica Francis akimsikiliza mkurugenzi mkuu Ruwasa Mhandis Kivegalo.
Meneja wa Ruwasa mkoa wa Shinyanga aliyesimama Mhandisi Julieth Payovera akitoa utambulisho kwenye kikao.
Mwenyekiti wa jumuiya ya chombo cha watumia maji kijiji cha Ng'washi kata ya Pandagichiza Magreth Magina akizungumza kwenye kikao. Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464