Suzy Luhende, Shinyanga Blog
Kanisa la Philadelfia Miracle Temple lililopo kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga limetoa msaada wa madaftari, kalamu na vifuto kwa watoto wanaoishi mazingira magumu 36 ambao wanaishi katika mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga.
Akikabidhi msaada huo mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Anania Clementi kwa niaba ya Askofu wa kanisa hilo Laizer Baraka amesema msaada huo wa vifaa vya shule vitawasaidia wanafunzi kwaajili ya kuandika masomo mbalimbali ambayo watafundishwa darasani ili waweze kufaulu na kutimiza ndoto zao.
Mchungaji Anania ambaye pia ni mjumbe wa serikali za mtaa katika mtaa wa Butengwa amesema msaada huo uliotolewa na kanisa ni mwendelezo, kwani kanisa hilo baada ya kutoa msaada wa awali liliahidi tena kutoa madaftari kalamu kwa wahitaji wanaosaidiwa na kanisa la Philadelfia.
"Vifaa hivi tulivyovitoa tunawaomba mkavitunze vizuri ili mtakapofungua shule muweze kutumia, pia tunawaomba wazazi na walezi muwatunzie hawa watoto wasiharibu haribu ili watakapofungua shule mnawapatia awamu kwa awamu na kuhakikisha wanaandika vipindi vyote vinavyofundishwa shuleni," amesema Anania.
Kwa upande wake mama askofu wa kanisa hilo Evaline Msangi wakati akigawa msaada huo kwa watoto amewaomba wazazi na walezi wawasimamie watoto hao, wawalee katika maadili mema ya kumpendeza Mungu na kuwaepusha na makundi mabaya ili waweze kuendelea na masomo ya juu baadae waweze kujitegemea na kuwasaidia.
"Kanisa la Philadelphia limeamua kuwasaidia watoto hawa wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao waweze kujisikia vizuri kama watoto wengine, hivyo tutakuwa bega kwa bega, pale Mungu atakapotuwezesha tutaendelea kuwasaidia, tunawaomba na wadau wengine ambao wataguswa kuwasaidia watoto hawa tunawakaribisha na Mungu atawabariki,"amesema Evaline.
Elizabeth Martine mkazi wa mtaa wa Butengwa ameshukuru kwa kuendelea kusaidiwa wajukuu wake, kwani anaishi na wajukuu wanne ambao wazazi wao hawapo wameenda kutafuta kazi sehemu mvalimbali hivyo alikuwa hana uwezo wa kununua madafutari na kalamu, lakini kwa sasa kanisa limesaidia Mungu aliinue na awabari wote waliojitoa.
Mama Askofu Evaline Msangi akikabidhi vifaa vya shule kwa mwanafunzi wa chekechea
Kazi ya kigawa vifaa kwa watoto wa mtaa wa Butengwa ikiendelea
Mchungaji msaidizi wa kanisa la Philadelfia Anania Clementi akizingumza na mtoto baada ya kukabidhi daftari na Kalamu
Mchungaji msaidizi wa kanisa la Philadelfia Anania Clementi akizingumza na watoto pamoja na wazazi na walezi
Watoto wakiendelea kugawiwa vifaa vya shule