Katibu wa Oganaizesheni umoja wa wazazi Taifa jumuiya ya chama cha mapinduzi CCM Said King'eng'ena akitoa semina elekezi kwa viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga
Suzy Luhende,Shinyanga blog
KATIBU wa Oganaizesheni umoja wa wazazi Taifa jumuiya ya chama cha mapinduzi CCM Said King'eng'ena amewakumbusha viongozi wa chama cha mapinduzi CCM mkoa na jumuia zake kuimalisha mashina ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na kusoma katiba ya chama cha mapinduzi CCM, ili kuhakikisha chama kinasimama imara na kuleta ushindi.
Licha ya kuimalisha mashina pia amewataka makatibu tawi na kata kuanzia kesho waanze kutembelea mashina yao ya chama ili kujua changamoto zilizopo na kuweza kuzitatua kwa wakati na kuwa na mazoea ya kusoma katiba ya chama, ili kuweza kukisimamia vizuri chama hicho pamoja na kuweka pembeni makundi yaliyotokana na uchaguzi na kuwa na mahusiano mazuri.
Hayo ameyasema leo kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM yaliyoandaliwa na jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga na kufanyika katika kata ya Solwa halmashauri ya Shinyanga wakati akitoa semina elekezi kwa viongozi kuanzia mashina hadi mkoa, ambapo pia yaliambatana na upandaji miti katika shule ya sekondari Solwa.
King'eng'ena amesema mwenyekiti na katibu wakishirikiana kwa pamoja na kuimalisha mashina yote na kutatua changamoto zote zilizopo, lazima ushindi utapatikana na kila kiongozi anatakiwa kumjua balozi wake na kujua namba ya shina lake.
"Niwaombe sana viongozi wenzangu ili kukiimalisha chama chetu na jumuia zetu ni vizuri mkaondokana na makundi mliyokuwa nayo kwenye uchaguzi, muwe na mahusiano mkashirikiana na wenyeviti wenu wa mashina katika kuwasaidia kutatua kero mbalimbali,pia aliwaomba kila kiongozi ajue wajibu wake wa kazi,"amesema King'eng'ena.
Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga alishukuru kwa elimu iliyotolewa na katibu Oganaizesheni, hivyo wataifanyia kazi na watayazingatia yote waliyofundishwa, hivyo haya yote tukayatekeleze na kuhakikisha tunaendelea kushika dola.
"Tunakushukuru sana kiongozi wetu kwa kutufunda sisi viongozi, hivyo maelekezo yote uliyoyatoa tutayatekeleza na tutafanya kazi zetu kwa kufuata utaratibu wa kazi na kuhakikisha tunaboresha zaidi"amesema Katibu wa jumuia ya wazazi Rejina Ndulu.
Naye mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum ameshukuru kwa elimu aliyoipata hivyo wamejua mengi na wataendelea kuyafanya na kuyasimamia ipasavyo ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinazidi kushika dola.
Katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga akimpa taarifa ya hali ya uongozi na hali ya siasa na mahusiano katibu wa Oganaizesheni kutoka jumuia ya wazazi Taifa Said King'eng'ena
katibu wa Oganaizesheni kutoka jumuia ya wazazi Taifa Said King'eng'ena akiendelea kutoa elimu kwa viongozi
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salumu akiwa na viongozi wa chama na jumuia zake wakimsikiliza katibu akiendelea kutoa elimu
Viongozi wa chama na jumuia zake wakiendelea kumsikiliza katibu wa Oganaizesheni kutoka jumuia ya wazazi Taifa Said King'eng'ena
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje akizungumza baada ya kuelimishwa mambo ya uongozi
Katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akishukuru kwa mafunzo aliyoyapata
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya lizaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akishukuru maelekezo yaliyotolewa na
katibu wa Oganaizesheni kutoka jumuia ya wazazi Taifa Said King'eng'ena