MWENYEKITI WAZAZI AWATAKA MAKATIBU ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA KUTOA ELIMU YA MALEZI MASHULENI IKIWA NI PAMOJA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO WANAFUNZI




Suzy Luhende, Shinyanga blog

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga John Siagi amewataka makatibu elimu malezi na mazingira kutoa muda wa kutembelea mashuleni kwa ajili ya kutoa elimu na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo watoto, huku akiwataka viongozi wa jumuia kuanzia matawi kata wilaya kuanzishe miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi.

Agizo hilo amelitoa leo kwenye maadhimisho ya kufikisha miaka 46 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi CCM yaliyoandaliwa na jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga, ambapo wameadhimisha kwa kukagua soko la mitumba linalojengwa kata ya Ngokolo na kukagua shule ya sekondari ya wasichana mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga.

Siagi amesema wanapoadhimisha miaka 46 ya chama cha mapinduzi CCM ni vizuri wakawakumbuka watoto, kwani wanakutana na changamoto nyingi inawezekana hawajui pakuzipeleka waelimishwe, lakini jumuia ya wazazi kwa vile wamepewa jukumu la malezi ni vizuri kusimamia na kujua maendeleo ya watoto, kwani kuna wengine wanafanyiwa ukatili wa kubakwa wengine kulawitiwa.

"Jumuia ya wazazi tuna jukumu kubwa la kuwafundisha maadili na kufundisha malezi mema watoto wetu, hivyo viongozi wote tusikae maofisini tutenge muda wa kuwatembelea mashuleni watoto wetu tuwafundishe malezi mema na maadili yanayotakiwa ili tuwe vijana wanaojitambua na kuweza kulitumikia Taifa letu,"amesema Siagi.

"Pia tunahitaji jumuia yetu iwe na wanachama wengi zaidi viongozi wote kuanzia ngazi ya matawi tunatakiwa tuongeze wanachama kila kiongozi afanye mchakato wa kuhakikisha anaongeza wanachama katika jumuia ya wazazi tupendane tusiendeleze makundi ambayo hayajengi chama," ameongeza Siagi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Fue Mlindoko amesema  kuna watoto wengi wa kiume wanatembea upande upande kwa ajili ya kulawitiwa, hali inakuwa ni mbaya sana kwa watoto wa kiume ni vizuri kuanzia mashuleni ili kuhakikisha hiyo hali haiendelei.

"Kwa sasa maadili yamepungua kwenye jamii utakuta mtoto ana umri wa miaka nane, 10, 11 anarudi saa nne ya usiku, hali ambayo anaweza kufanyiwa kitu kibaya ikiwemo kubakwa na kulawitiwa, hivyo tabia hiyo tunatakiwa tuipinge kwa sauti moja tusikubali tuwalaani wote wanaofanya vitendo hivi," amesema Mlindoko.

Naye katibu wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amewaomba wazazi  na walezi wawape malezi mema watoto wao na kuwasisitiza kuzingatia masomo, kwani kila familia yenye maendeleo ina watoto waliosoma bila elimu hakuna maendeleo watoto wote wana haki ya kusoma.

"Leo tumekuja kukagua shule ya sekondari ya wasichana hivyo wanatakiwa kuletwa mahali hapa ili waendelee na masomo, unakuta mtoto anabebeshwa mimba mzazi na mzazi wanaelewana tukiwabaini tutawachukulia hatua kali za kisheria,  na sisi tunachukua jukumu la kuwasaka watoto wa kike waingie darasani,"amesema Kibabi 

"Niwaombe wazazi usimwamini mtu wala jirani juu ya mtoto wako unaweza ukamwamini kumbe ndiye anayeharibu mtoto wako, hapa Shinyanga kuna wimbi la wanaume mashoga, tukizembea kwa baadae tutakosa wanaume waume wanaozalisha, hivyo tunatakiwa tuwalinde na tuwachunguze watoto wetu jamani, amesisitiza Kibabi.

Pia amesema kuna wazazi wanawaambia watoto wa kike wakadange wawaletee chipsi, hali ambayo inaweza kumsababishia mtoto huyo akapata mimba, magonjwa na baadae utakosa mtoto wa kukusaidia, hivyo tuwahimize kwenda shule, inauma sana kuona mtoto wa kiume amebadilika na kuwa shoga na huku ulimzaa akiwa mzima,"amesema Kibabi.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Anord Makombe amesema hii shule inayoendelea kujengwa inatakiwa ifanyiwe haraka ili watoto weweze kuanza masomo hivi karibuni wasiendelee kukaa majumbani hawa wanafunzi 120 waanze masomo.

Ofisa elimu sekondari Cleoface Mzungu amesema wanafunzi 120 wakike wameandikishwa katika shule hiyo, bweni moja linaweza kuchukua wanafunzi 20 na tayari bweni tano zimejengwa na kuezekwa.
Katibu wa jumuia ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi akinawa baada ya kupanda mti katika shule ya sekondari ya wasichana Butengwa manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga kushoto John Siagi akipanda mti katika shule ya sekondari ya wasichana Butengwa manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Anord Makombe akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 yachama cha mapinduzi CCM

Ofisa elimu sekondari Cleoface Mzungu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya chama cha mapinduzi CCM

Viongozi na wananchi wa Shinyanga mjini wakiendelea kukagua majengo ya shule ya sekondari ya wasichana iliyopo mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga

Viongozi na wananchi wa Shinyanga mjini wakiendelea kukagua majengo ya shule ya sekondari ya wasichana iliyopo mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga

Viongozi na wananchi wa Shinyanga mjini wakiendelea kukagua majengo ya shule ya sekondari ya wasichana iliyopo mtaa wa Butengwa manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi jumuia ya wazazi mkoa akiwa na viongozi wa jumuia hiyo katika maadhimisho ya mika 46 ya chama cha mapinduzi CCM


Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga akizungumza


Katibu wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi akiwa ameongoza jopo la viongozi wakiendelea kukagua shule ya sekondari ya wasichana

Viongozi wakiendekea kukagua



Viongozi wa chama na wananchi wakimsikiliza mwenyekiti wa jumuia ya wazazi Mkoa Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464