Na Kareny
Masasy, Shinyanga
MKURUGENZI mkuu wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) Mhandisi Clement Kivegalo amesema Makampuni ya wakandarasi wazalendo wanaotekeleza miradi ya maji nchini
wenye kufanya vizuri wapewe cheti cha kutambuliwa na pongezi.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 13/07/2023 kwenye ziara yake mkoani hapa alipotembelea utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Ishinabulandi kata ya Samuye
nakukagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 100,000 na mnara wa mita 12.
Mhandisi
Kivegalo amesema mradi wa maji unaotekelezwa kijiji cha Ishinabulandi umefikia asilimia 37 unaenda vizuri hivyo
mkandarasi wa kampuni ya Mbesso
Construction hajachukua fedha ya
serikali yoyote mpaka sasa ametumia yakwake.
Mhandisi
Kivegalo amesema wakandarasi wa namna hiyo
ni wazalendo ofisi za Ruwasa mkoa
ziwaandalie cheti cha pongezi na
chakumtambua ili anapoomba tena kazi aweze kufahamika nakupewa tena.
Mhandis
Kivegalo amewapongeza Ruwasa mkoa na wilaya kwa kazi nzuri wanazozifanya sanjari na
jumuiya ya watumia maji (CBWSO )iliyopo kata ya Ukenyenge wilayani
Kishapu kwa kuwa na ofisi na ukusanyaji mzuri wa mapato.
Mhandisi
Benjamin Pares msimamizi wa kampuni hiyo ameomba kuongezwa muda kwa kuchelewa
kuanza kazi huku changamoto akieleza ni ucheleweshaji wa kupata vifaa ikiwa asilimia kubwa anatumia mabomba na
unatarajia kukamilia mwezi Februari mwaka huu.
Meneja wa
Ruwasa wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emaeli Nkopi amesema mradi huo unatarajia kuhudumia vijiji nane
ambavyo ni Ishinabulandi,Idodoma,Isela.Ibingo.Ng’wahalanga,Mwamala
na Ibanza.
“Mradi huo
unagharimu sh Billioni 4.7 ambapo kunajengwa
matanki mawili moja Ishinabulandi
na lingine kata ya Mwamala lenye ujazo wa lita 200,000 nakuhudumia watu 23,000.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya watumiaji maji Kassimu
Kishiwa amesema mradi huo
umewasaidia hata baadhi ya akina mama
kwenye familia ndoa zao kudumu kwani walikuwa
wanatafuta maji nakuachika.
Mtendaji wa jumuiya hiyo Hassan Alfan amesema wanahudumia vijiji 15 na mafanikio mpaka sasa wamejenga kituo cha kutolea maji kwa fedha za makusanyo na ofisi ya Ruwasa wilaya ya Kishapu iliwakabidhi pikipiki mbili
Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa nchini Mhandisi Clement Kivegalo akiwa na meneja wa Ruwasa Mkoa Julieth Payovera pamoja na meneja wilaya ya Kishapu Mhandis Dickson Kamazima.
Wakwanza kushoto ni meneja Ruwasa wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emael Nkopi katikati ni mkurugenzi mkuu wa Ruwasa nchini Mhandisi Clement Kivegalo na pembeni yake meneja Ruwasa mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.