Na Kareny Masasy,Shinyanga
JUMUIYA ya umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Shinyanga vijijini wamesherekea miaka 46 za kuzaliwa kwa chama hicho huku wakifanya shughuli za upandaji miti nakutembelea wodi ya wazazi katika kituo cha afya Iselamagazi.
Zoezi la
upandaji miti liliongozwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya
Shinyanga vijijini Edward Ngelela jana kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye mbunge
wa jimbo la Solwa Ahamed Salum.
Ngelela pia
aliongoza viongozi wa jumuiya hiyo kutembelea wodi ya wazazi ambapo walijionea huduma zinavyotolewa kwenye
kituo hicho nakuwataka watumishi waendelee kuvumilia changamoto na kutotoa
lugha za matusi kwa wazazi.
Ngelela
amewataka UWT kuhakikisha kiwanja ambacho wamekionyesha leo na kupandwa miti
kisimamiwe na kupata hati miliki.
Aidha mganga
mfawidhi wa kituo cha afya Iselamagazi dk Daniel Singolile amesema changamoto iliyopo ni
msongamano wa wagonjwa ambapo hukitumia kama
kupata rufaa kwenda hospitali ya wilaya.
Katika
sherehe hizo diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema amesema serikali imetekeleza ilani ya uchaguzi kwa vijiji vyote kupata
huduma ya maji.
“Kata hii
imepata neema kubwa kwa kupokea zaidi ya
sh Billioni tatu katika kutekeleza
miradi ya maendeleo na ujenzi wa Zahanati unakamilika kwenye kijiji cha
Mwabundala”amesema diwani Sengerema.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Mecktilida Mkali akipanda mti siku walipoadhimisha miaka 46 tangu kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika eneo la kituo cha afya Iselamagazi wakisubiri maelekezo ya kuwaona wazazi nakuwapa zawadi.
Viongozi wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini wakiongozwa na mweyekiti wa chama hicho wilaya Edward Ngelela aliyevaa shati la kijani wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mganga mfawidhi wa kituo cha afya Iselamagazi ambaye hayupo pichani
Viongozi wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini wakiwa na watumishi wa kituo cha afya Iselamagazi wakionyesha moja ya zawadi walizokuwa nazo.
Mzazi Felister Mihambo akiwa wodi ya wazazi kituo cha afya Iselamagazi akipata pongezi kutoka kwa viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini pamaja na uongozi wa UWT.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela akimpa zawadi ya sabuni mzazi Sara Richard aliyejifungua kwenye kituo cha afya Iselamagazi.
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini akiwatambulisha wanawake wa jumuiya hiyo kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Ernestina Richard kushoto kwake ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Khamis Salum akijitambulisha kwenye mkutano wa hadhara.
Katikati ni diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela na kulia ni katibu wa chama hicho Ernestina Richard wakiwa meza kuu.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Ernestina Richard akipanda mti kwenye kiwanja cha UWT kilichopo kata ya Iselamagazi. Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464