UWT YALAANI KUENDELEA KWA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO



Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa UWT Hellen Bugohe akikata keki

Suzy Luhende Shinyanga Blog

MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa UWT Hellen Bugohe amelaani vikali kuendelea kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto pamoja na ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume, ikiwa ni pamoja na kuwataka viongozi kuwa na ushirikiano katika kukijenga chama.

Pia amewataka wazazi kuacha kuficha pindi watoto wao wanapolawitiwa na kubakwa badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya dola na wajenga tabia ya kulinda  usalama wa watoto wao ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili huo.

Akizungumza jana kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM yaliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa CCM Mkoa wa Shinyanga, yaliyofanyika wilayani Kishapu mkoani hapa, amesema kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii hali ambayo imekuwa ikisababisha ukatili mkubwa kwa watoto na wakubwa.

Bugohe amesema wazazi wengi wamekuwa hawawafuatilii watoto wao, wamekuwa wakiwaachia kwenda kuangalia mpira baadala ya kuangalia mpira wamekuwa wakionyeshwa picha za ajabu kwenye vibanda vya video, hivyo wazazi wanatakiwa kufuatilia watoto wao kwa karibu watokapo na waingiapo.

Nawaombeni wazazi msiwe bize na maisha ili watoto wetu wa kike na wa kiume waweze kuwa salama tunatakiwa tujenge tabia ya kuwa karibu nao, tuwaogeshe wale wenye umri mdogo i
na tuwakague ili kuona kama wamefanyiwa vitendo vya ubakaji, ama kulawitiwa ukimshika sehemu za siri na kuona anarudi nyuma tambua kuwa tayari amefanyiwa ukatili ,”amesisitiza Bugoye.

"Tunapata wageni wajomba binamu na kuwalaza chumba kimoja na watoto wetu wadogo, kwani kila mtu anatabia yake hivyo usimwamini anaweza akawa ameshakengeuka akamfanyia vibaya mtoto, tunatakiwa kuwa makini sana wazazi wenzangu, tuepuke hicho kitendo tuwe tuna watenga wageni sehemu yao na watoto kwenye chumba chao sababu hawasomeki,"ameongeza Bugoye.

"Kuna baadhi ya kina baba wamekuwa na tabia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto wao, tabia hiyo ni mbaya sana tunaikemea na kuilaani isiendelee kujitokeza, tunapoona hivyo sisi wanajanajamii tutoe taarifa mapema ili mtu huyo achukuliwe hatua,"amesema Bugoye.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli aliwashukuru wanachama wote wa jumuia zote za CCM waliofika katika maadhimisho hayo na kuwaomba yale yote yaliyosemwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa UWT wakayafanyie kazi na wakawe mabalozi kwa wananchi ambao hawakufanikiwa kufika katika maadhimisho hayo.

"Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa ametusihi  wanashinyanga tukijenge chama chetu tushirikiane kwa pamoja tuachane na wapambe ambao wataweza kutugombanisha tukashindwa kushirikiana na tumuunge mkono Rais wetu kwa kazi anazozifanya" amesema Grace

Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kishapu Rahel Madundo amewataka wazazi na walezi wawaruhusu watoto waliofaulu kidato cha nne kwenda shule ili wasome na kutimiza ndoto zao kwani ndiyo tegemeo la familia na Taifa, wasipofanya hivyo ni kuwafanyia ukatili watoto hao.

Katika sherehe hizo za miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, Umoja huo wa wanawake UWT, pia umeadhimisha kwa kupanda Miti katika Hospitali ya Jakaya Kikwete wilayani Kishapu, pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa katika Hospitali hiyo zikiwamo sabuni za kufulia, biskuti,mafuta ya kupaka na Juice.

Baadhi ya Wagonjwa akiwamo Grace Dotto amewashukuru wanawake hao wa UWT kwa kuwapatia msaada zawadi hizo, nakuwapongeza kwa huduma za matibabu ambazo wanapewa katika Hospitali hiyo,na kudai kuwa baada ya kutoka hospitali ataenda kuchukua kadi ya CCM na UWT kwa sababu ameona chama hicho kinajali watu wake.

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Jakaya Kikwete wilayani Kishapu Dkt. Mohamed Mkumbwa, amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha na kuboresha huduma za matibabu katika Hospitali hiyo, ambapo amesema serikali ya mama Samia Suluhu imeleta vifaa mbalimbali na dawa za kutosha katika hospitali hiyo.


Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa UWT Hellen Bugohe katikati akiwa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake Grace Samweli kushoto ni katibu wa 


Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa UWT Hellen Bugohe akizungumza kwenye Maadhimisho  ya  CCM

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Samweli akizungumza kwenye maadhimisho hayo


Katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Shinyanga Halima Makoroganya akozungumza kwenye maadhimisho ya miaka  46 ya kizaliwa kwa CCM



Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akizungumza kwenye sherehe hizo


Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa Hellen Bugohe akiwa amebeba mtoto baada ya kutoa zawadi katika hospitali ya wilaya ya Jakaya Kikwete 


Mjumbe wa Baraza la wanawake Taifa Hellen Bugohe akitoa kadi kwa wanachama wapya wa UWT



Katibu msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Halima Makoroganya akipokea zawadi kutoka kwa wanawake wa Kishapu


Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Samweli akipokea zawadi kutoka kwa wanawake wa WUT Kishapu

Katibu wa UWT Bi Mauwa akizungumza



Mjumbe wa baraza la wanawake Hellen Bugohe  akigawa kadi kwa wanachama wapya wa UWT



Ndelemo na vifijo vikiendelea 

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya Ally Majeshi akilishwa keki na mjumbe wa baraza Taifa



Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Samweli akimwagilizia mti baada ya kuupanda akisaidizana na wajumbe wake kulia ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Namanilo

Mjumbe wa baraza la  UWT Taifa Hellen Bugohe akimwagilia mti baada ya kuupanda


Katibu wa UWT Wilaya ya Kishapu Rahel Madundo akisalimiana na mjumbe wa baraza Taifa Hellen Bugohe

Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa  katikati akiwa na mwenyekiti wa UWT mkoa Grace Samweli na katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464