WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWALINDA WATOTO WA KIUME ILI WASIJIINGIZE KWENYE USHOGA

Katibu wa Oganaizesheni  jumuiya ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena akiendelea kukagua shule ya sekondari Solwa


Suzy Luhende,Shinyanga Blog

KATIBU  wa Oganaizesheni  jumuiya ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena amewataka wazazi na walezi kulea katika maadili mema watoto wa kiume ili wasijiingize kwenye ushoga, na baadae wakakosekana wanaume lijali.

Hayo ameyasema jana kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM yaliyoandaliwa na jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga na kufanyika katika kata ya Solwa halmashauri ya Shinyanga, ambapo amesema kuna baadhi ya watu wanafundisha mambo ya ushoga, hivyo ni kuwa makini kuwalinda watoto wasijiingize kwenye mambo hayo.

King'eng'ena amesema jukumu la jumuiya ya wazazi ni kufundisha malezi mema  na maadili kwa watoto na kuweka mazingira katika hali nzuri, kupanda miti na kuitunza ili isikauke ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

"Kuna baadhi ya watu wanajihusisha na mambo ya ushoga ambayo sisi watanzania hatuna utamaduni huo, tabia hii sio nzuri,  hivyo niwaombe sana wazazi na walezi tulinde watoto wetu na tuwaeleze madhara yake wasijiingize kwenye masuala hayo, tukemee tabia hiyo haifai hata kidogo, kwani tukizembea baadae tutakosa wanaume rijali, amesema King'eng'ena.

Amesema kazi ya chama cha mapinduzi ni kutatua shida za watu na kutatua kero zote zilizopo katika jamii, kutengeneza miundombinu ya barabara umeme na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji na huduma za afya sio chama cha kupiga kelele na kutukana.

"Hivyo kazi yetu kubwa ni kuomba dola na tuunge mkono chama chetu, kwa sababu kila kitu kinachofanyika kinaonekana kuna madarasa, kuna maji Zahanati na barabara zimetengenezwa na  zinaendelea kutengenezwa katika awamu hii ya sita, hivyo tunacha kusemea na kazi yetu kwa sasa ni kutafuta ushindi wa madiwani,wabunge na Rais tu,amesema King'eng'ena.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum amesema katika jimbo lake utekelezaji wa irani ya chama cha mapinduzi unaendelea miradi mbalimbali inatekelezwa madarasa yamejengwa miundombinu ya barabara ikiwemo maji safi na salama ambapo toka aingie bungeni mwaka 2005 kulikuwa na vijiji 17 ambavyo vilikuwa na maji lakini kwa sasa kuna vijiji 69 na vijji 22 vipo kwenye utekelezaji.

Mbunge Ahamed amesema katika kuhakikisha vijiji vyote vina pata maji kuna vijiji 21 vipo kwenye mpango wa Ruwasa fedha zipo, hivyo  kufikia mwezi wa 10 mwaka huu vitakuwa vijiji 89 hivyo wataondokana na tatizo la maji na mpaka sasa watavuka lengo la chama cha mapinduzi na mwaka 2024 watafikia asilimia 95

"Sasa hivi naenda awamu ya nne, katika utekelezaji wa mheshimiwa Rais wetu tumefanya kazi kubwa sana ukichukua takwimu ya maendeleo yaliyofanyika jimbo la Solwa linaweza likawa ni la 10 bora kwa maendeleo, hivyo tuendelee kumuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu aendelee kutuletea fedha za kutosha ili kila kijiji kipate huduma za kijamii zinavyotakiwa"amesema Ahamed.

Aidha mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi amesema shabaha ya chama hicho ni kutetea wanyonge katika kutatua kero mbalimbali na kusimamia irani ya chama cha mapinduzi CCM, hivyo kinachotakiwa ni kuwaunga mkono viongozi wa Taifa kwa kuwapongeza kwa kazi kubwa wanazozifanya, hivyo kuna hoja za kuzungumzia.

"Wilaya ya Solwa kwa ushirikiano wenu ninawasihi sana tuendelee kukiunga mkono chama chetu kwa sababu tunaona maendeleo yanayofanyika na itafika mahali jimbo hili linakuwa jiji  kwa maendeleo yanayofanyika mahali hapa, tuendelee kupambana ili kuhakikisha jamii yetu inapata huduma zote za kijamii zinazotakiwa,"amesema Siagi.


Katibu wa Oganaizesheni jumuiya ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama chamapinduzi CCM yaliyoandaliwa na jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga


Mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya chama cha mapinduzi CCM

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM

Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi CCM


Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga akisalimia wananchi kwenye maadhimisho ya miska 46 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi CCM


Wanachama na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza katibu wa Oganaizesheni jumuia ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama chamapinduzi CCM


Wanachama na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Shinyanga wakimpungia mkono katibu wa Oganaizesheni jumuia ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama chamapinduzi CCM

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza


Mjumbe wa baraza la wazazi Taifa Edwin Nkenyenge akipanda mti katika viwanja vya shule ya sekondari Solwa


Mjumbe wa baraz la wazazi mkoa wa Shinyanga akipanda mti katika shule ya sekondari Solwa


Wanachama wa chama cha mapinduzi CCM wakipanda mti katika viwanja vya shule ya Sekondari Solwa



Katibu wa jumuia ya wazazi mkia wa Shinyanga Rejina Ndulu akinawa baada ya kupanda mti katika shule ya sekondari ya Solwa



Wanachama na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Shinyanga wakimsikilza katibu wa Oganaizesheni jumuia ya umoja wa wazazi Taifa Said King'eng'ena akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama chamapinduzi CCM
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464