Moja ya wanafunzi wa darasa la awali wakiwa kwenye hali ya ujifunzaji.
Na Kareny
Masasy
Tanzania ni
nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki katika elimu ya awali kuifanya kuwa ya lazima
kwenye sera ya elimu na mafunzo ya mwaka
2014.
Aidha
uandikishwaji wa elimu ya awali nikiashiria
muhimu kilichongizwa katika mpango
wa taifa wa maendeleo ya miaka mitano 2016/17-2020/21.
Saada Robert mkazi wa kitongoji cha Mwashagi kijiji cha
Lyabukande halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga mwenye watoto wawili mmoja anamiaka nane na mwingine miaka 6 amejitokeza kuandikisha watoto hao.
“Nimekuja
kuwaandikisha wanangu waanze darasa la
awali walichukuliwa na baba yao na kuwatelekeza nyumbani kwao
kijijini”anasema Robert.
Robert anasema
amewafuata mkoani Tabora baada ya kusikia hawasomi wanachunga mifugo ya bibi yao.
“Nilikasirika
sana kusikia wanangu hawasomi na baba yao kakalia ulevi tu…….”anasema Robert.
Sofia
Charles Mkazi wa kijiji cha Lyabukande anasema
ameona umri wa mtoto wake mwenye
miaka mitano unatosha kuanza darasa la awali
kama wanavyoelezwa na serikali aanze darasa la awali kwanza.
“Nimemleta
bila sare za shule nikipata pesa baadaye nitamnunulia ngoja kwanza aendelee
kujifunza”anasema Charles.
Pendo Mayala
anasema amekuja kumuandikisha mtoto wake mwenye umri wa miaka nane kuanza
darasa la awali sababu alikuwa akiishi na babu yake kijiji jirani.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Lyabukande Peter Labacha anasema wameweka mpango mkakati wa kuhakikisha kila
mzazi mwenye mtoto anayetakiwa kuanza
shule aanze.
“Baadhi ya wazazi
wameanza kuelewa wanawapeleka
shule watoto na majira ya saa tano wanapotoka
huwafuata hadi shuleni”anasema Labacha.
Mwalimu Nyebu Musa anayefundisha darasa la awali
shule ya msingi Lyabukande anasema wazazi wamepata mwamko wa kuleta watoto.
“Zipo mbinu
za ufundishaji wa watoto ili waendelee kuipenda
hawa ukiwakemea kesho darasa zima hawaji shule “anasema Mwalimu Musa.
Musa anasema
mara nyingi wamekuwa wakiimba nyimbo,kucheza na kusimulia hadithi ambayo wataifurahia.
Musa anasema
darasa moja lina wanafunzi 42
walioandikishwa mpaka sasa wasichana ni 22 na wavulana ni 20 hivyo takwimu hii
inaenda ikiongezeka kila siku za shule wanaripoti.
Musa anasema
mwaka jana walikuwa wanafunzi 150 darasa moja
wakianzia umri wa miaka minne hadi
nane.
‘Mwanafunzi
akionekana umri wake ni mkubwa hawamuweki darasa la awali anavukishwa kwenda darasa la kwanza kwa
matazamio ya kujua KKK”anasema Musa.
Musa anasema
wanaishukuru serikali kuhimiza watoto
walio na umri wa miaka minne waanze shule baadhi wenye miaka mitano wameingia
darasa la kwanza wakijua KKK.
Mwalimu mkuu
wa shule ya msingi Lyabukande Jeremiah
Mashaka anasema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1956 walikuwa hawana mwalimu wakufundisha darasa la
awali.
Mwalimu
Mshaka anasema baada ya sera kuelezwa kila shule iwe na darasa la awali
ikalazimika kutafuta mwalimu mwaka jana
aliyepitia mafunzo na kujitolea.
Mratibu
elimu kata ya Kyabukande Harun Ibrahimu
anasema kata yake ina vijiji saba na kila kijiji kina shule
ya msingi lenye darasa la awali.
Ibrahimu
anasema uandikishwaji wa watoto huwa
wanautangaza kwenye mkutano wa hadhara ili kila mzazi mwenye mtoto wa umri wa
kuanza shule andikishwe.
Ofisa elimu
msingi kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Christina Bukori anasema matarajio ya
uandikishaji wa darasa la awali ni watoto 11,136 na walioandikishwa mpaka sasa
ni watoto 10,122 sawa na asilimia 96.
Bukori anasema wazazi wamepata mwamko wa kuandikisha watoto shule kwa mwaka jana waliandikishwa watoto zaidi ya 10,000.
Mshauri wa malezi,makuzi na maendeleo ya
awali ya mtoto kutoka shirika la Children in Crossfire (CiC) Davis Gisuka anasema mtoto anapopata elimu ya
awali inamjengea uchangamfu na uelewa wa vitu mbalimbali kwake.
“Kuna faida
mtoto kuanza darasa la awali maana darasa la awali zaidi atajifunza nyimbo
zenye ujumbe,michezo na hadithi na mbinu
hiyo itamfanya kuweka kumbukumu na
kujua kuhesabu namba”anasema Gisuka..
Waziri wa
nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angela
Kairuki amesema mchakato wa uandikishaji
wa darasa la awali uendelee.
“Ninasema watoto wenye umri wa miaka minne hadi mitano waanze darasa la awali ili wawe na ufahamu mzuri darasani na kuondoa wanafunzi wasio jua KKK”anasema Kairuki.
Kwa mujibu
wa programu jumuishi ya Taifa ya malezi,makuzi
na maendeleo ya awali ya mtoto
PJT-MMMAM 2021/22-2025/26 inaeleza
kuwepo mazingira rafiki ya kisera kumepelekea ongezeko la uandikishwaji wa watoto.
Ndani ya mwaka mmoja umefikia uandikishaji 500,000 kutoka 1,069 823 mwaka 2015 mpaka 1,562,770 mwaka 2016.