Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga waadhimisha wiki ya sheria nchini.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akikagua Gwaride kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.
Na Halima Khoya na Kadama Malunde - Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati amewataka Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea wawasaidie wateja wao kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani inaleta tija ili kuondokana na mrundikano wa mashauri, kupunguza chuki, kuokoa muda kutekeleza shughuli za maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi endelevu badala ya kuwaacha watunishiane misuli Mahakamani.
Jaji Kilati ametoa rai hiyo leo Jumatano Februari 1,2023 wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga yakiongozwa na Kauli Mbiu inayosema “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau”.
Jaji Kilati amesema Mawakili ni wadau wakubwa kwa kesi za madai na jinai hivyo ni vyema wakajitahidi kumaliza mashauri kwa njia ya usuluhishi kwa wateja wao kufanya mazungumzo ili kumaliza kesi na kuokoa rasilimali zao pamoja na kuondoa tofauti za migogoro katika mioyo yao.
Pia amewataka wananchi na viongozi wa kiutawala waonapata kesi nyingi za migogoro watatue migogoro kwa njia ya usuluhishi.
“Mawakili wa serikali na kujitegemea wasaidieni wananchi kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kuwasaidia kuokoa muda wakatekeleze shughuli za uchumi, kujenga undugu, kusaidia jamii inayowazunguka kwani migogoro inaleta uadui na chuki. Msiwaache watunishiane misuli mahakamani, tunataka mpoze hiyo misuli”,amesema Jaji Kilati.
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga.
Amesema faida za utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni pamoja na migogoro kumalizika mapema na haraka, ni njia rafiki kwa wadau wote kumaliza mgogoro, inaondoa tofauti za kimigogoro na chuki, tofauti na shauri kupelekwa mahakamani na Wadau wote kwenye shauri wanakuwa washindi kwa sababu wanakuwa wameafikiana kwa pamoja.
“Mahakama inatakiwa itoe haki bila kuchelewesha kwani ni wajibu wetu kikatiba . Utatuzi wa migogoro kwa Usuluhishi ni njia ambayo wadau wote kwenye shauri huwa ni washindi tofauti na kupelekana mahakamani ambako kila upande hutunisha misuli ili kuibuka mshindi”,amesema.
Ameeleza kuwa Migogoro katika jamii inasababisha mdororo wa uchumi na ili kuwa na uchumi endelevu ni vyema njia za usuluhishi zitakatumika kumaliza mashauri akisisitiza kuwa Mahakama inasisitiza usuluhishi iwe kipaumbele cha kutatua migogoro ili kuokoa muda na rasilimali.
“Japo bado mwitikio wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ni mdogo kutokana na wananchi kutotambua umuhimu wa kumaliza kesi kwa kuafikiana. Tusiendeleze migogoro kiasi cha kuathiri uchumi kwani wapo watu wanapenda kutunishiana misuli mahakamani na kesi zinachukua muda mrefu kukamilika, tunapoteza muda”, amesema Jaji Kilati.
Katika hatua nyingine amesema Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imefanikiwa kumaliza mashauri ya Mrundikano ambapo hivi sasa hakuna hata shauri moja la mrundikano na inaendelea kumaliza mashauri ya kawaida
“Tunahitaji nguvu za pamoja kumaliza kesi hizi za kawaida ambapo njia nzuri ya kumaliza migogoro ni usuluhishi”,ameongeza Jaji Kilati.
Muonekano wa mbele jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Kwa upande wake, Wakili wa serikali Mwandamizi Solomon Lwenge amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wote kwa kuendelea kuongoza vyema katika kuwaletea maendeleo wananchi na hali bora ya maisha.
Amesema pamoja na kuwapata waendesha usuluhishi, majadiliano, maridhiano na upatanishi 494 nje ya maafisa wapatanishi ambao ni waheshimiwa mahakimu majaji wengine waliopo kwa mujibu wa sheria bado idadi ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya nchi.
“Uhalisia uliopo ni kwamba ukiondoa migogoro yenye asili ya madai iliyopo kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba na mahakama za mwanzo yapo zaidi ya mashauri 15,000 ya madai ya aina mbalimbali ambayo hayajaisha katika mahakama za mahakimu na zile za juu yake”,amesema Lwenge.
“Hivyo kwa mazingira haya naamini wakati umewadia wa kuboresha tena sheria ya mwenendo wa madai sura ya 33 ili shauri la madai lipate sifa ya kusajiliwa mahakamani endapo kuna uthibitisho kwamba limepita hatua ya usuluhishi”,ameongeza Lwenge.
Amesema Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali zitaendelea kusimamia vyema kwa niaba ya serikali matakwa ya sheria ya kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Moses Chilla aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amesema serikali imeweka madawati ya kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi na mirathi kwa njia ya usuluhishi ili kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na upendo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea (TLS) Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, Shaban Mvungi amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini kwa kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara huku akiwahamasisha Mawakili wa kujitegemea na Serikali kuongeza kasi ya kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani migogoro inakwamisha maendeleo na kuongeza uadui katika jamii hivyo ni vyema migogoro ikatatuliwa nje ya mahakama.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Sheria akiwemo Simon Mboje na Rehema Chimiyu wamesema utatuzi wa migogoro kwa njia kutasaidia kuondokana na adha ya kesi kuchukua muda mrefu huku wakiwaomba baadhi ya mawakili wasio waaminifu kuacha udanganyifu na kuendekeza tamaa ya pesa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga, Seif Mwinshehe Kulita akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Warsha Silvester Ng'humbu akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 1,2023 katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Moses Chilla aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, Shaban Mvungi akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wakili wa serikali Mwandamizi Solomon Lwenge akizungumza wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma Kilati akikagua Gwaride wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Kwaya ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ikitoa burudani wakati wa Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Wafanyakazi wa Mahakama wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga

Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yakiendelea.
Mahakimu wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yakiendelea
Wadau wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga.
Msanii Chap Chap akitoa burudani kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakisoma shairi kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga yakiendelea.
MC Amos Events maarufu MC Mzungu Mweusi akisherehesha Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Shinyanga
Picha ya kumbukumbu kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria

Picha ya kumbukumbu kwenye Kilele cha madhimisho ya Wiki ya Sheria.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog na Marco Maduhu.