MAOFISA UGANI SHINYANGA WAPEWA PIKIPIKI, WAONYWA KUZITUMIA BIASHARA YA BODABODA


Hafla ya ugawaji Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga imewapatia Pikipiki Maofisa Ugani mkoani humo, ambazo watazitumia kwa usafiri na kwenda kutoa elimu ya Kilimo cha kisasa kwa wakulima na kufanya kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa leo Februari 10, 2023 kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo jumla ya Pikipiki zilizogawiwa ni 221 kwa Mofisa Ugani katika wilaya tatu, Kahama Pikipiki 100, wilaya ya Shinyanga Pikipiki 82 na Kishapu Pikipiki 39 huku Pikipiki tatu zikibaki Mkoani.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Pikipiki hizo, amewataka Maofisa Ugani wakazitumie kwa madhumuni yaliyokusudiwa na siyo kwenda kuzianyia Anasa ikiwamo kuzifanyia biashara ya Bodaboda.

Amesema lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Pikipiki hizo kwa Maofisa Ugani ni kutaka kuona Sekta ya kilimo inaongeza uchangia katika Pato la Taifa, hivyo matarajio ya Mkoa katika Pikipiki hizo ni kuona uzalishaji wa mazao unaongezeka kwa wakulima sababu watakuwa wakitembelewa mara kwa mara na wataalam na kupewa elimu ya kilimo cha kisasa.

“Mofisa Ugani kazitumieni Pikipiki hizi kusaidi wananchi ili walime kilimo cha kisasa chenye Tija na siyo kwenda kuzitumia kwa mambo ya Anasa ikiwamo kuzifanyia Biashara ya Bodaboda,”amesema Dk. Nawanda.

Aidha, amewataka Mofisa Ugani mkoani Shinyanga wakaanzishe Mashamba darasa angalau kulima Hekali hata moja, ili Wakulima wapate kujifunza kutoka kwao, na kwamba yeye mwenyewe amekuwa pia akilima mashamba huko mkoani Simiyu na amelima Hekali 10, Tano za zao la Pamba na Hekali Tano kilimo cha Mahindi.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha Sekta ya kilimo na kutoa Pikipiki hizo kwa Maofisa Ugani, ambazo zitatumika kwa usafiri na kuwafikia wakulima kwa wakati na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na chenye Tija.

Nao Maofisa Ugani akiwano wa Kishapu Godwin Evalist, wamesema wanashukuru kupewa usafiri huo wa Pikipiki, ambao utawasaidia kuwafikia wakulima kwa wakati na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji wa mavuno na kuinuka kiuchumi.

Wakuu wa wilaya mkoani humo, wamesema Pikipiki hizo watazisimamia vizuri ili zikatekeleze madhumuni yaliyokusudiwa na Rais Samia ya kuinua Sekta ya kilimo.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Hafla ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Anold Makombe akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Wakurugenzi wa Halmashauri wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki za Maofisa Ugani Mkoani Shinyanga.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Hafla ya makaidhiano ya Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga ikiendelea.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Viongozi wakiziwasha Pikipiki na kuziendesha.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (kulia) akishikana Mkono na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kumkabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani wilayani Kishapu.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (kushoto) akishikana Mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kumkabidhi Pikipiki za Maofisa Ugani wilayani Shinyanga.
Muonekano wa Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.

Muonekano wa Pikipiki za Maofisa Ugani mkoani Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464