TAKUKURU SHINYANGA YABAINI UPOTEVU MAPATO MASOKO YA MANISPAA YA KAHAMA , MADUDU SEKTA YA AFYA

Takukuru wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari
 
Na Estomine Henry, SHINYANGA 
 
Takukuru Mkoa wa Shinyanga imebaini hali ya upotevu wa Mapato ya serikali katika manispaa ya kahama baada ya kufanya uchambuzi wa mfumo katika Halmashauri ya wilaya ya ushetu, manispaa ya kahama katika kipindi cha oktoba na desemba ,2022.

Hayo yameelezwa leo februari,16,2023 na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Bw.Donasian Kessy katika Mkutano wake ba vyombo ya habari mkoa wa Shinyanga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023(Oktoba-disemba,2022)

Kessy amesema,Takukuru ifanya uchambuzi wa mfumo kuhusu fedha za serikali katika mfumo wa upangishaji wa vibanda na meza za biashara katika Masoko ya manispaa ya Kahama na kubaini baadhi ya watendaji wa serikali kwa kushirikian na kamati za Masoko kuhodhi vipanda na meza kwa kutumia majina mengine na na kisha kupagisha kwa bei ya juu.

Pia kessy amesema zipo changamoto kwa manispaa hiyo kama,kamati kukusanya ushuru kwa kutumia risiti za mikono badala ya POS,mikataba ya taka kutojulikana kwa kamati za soko,masoko kutokujua kiasi cha bajeti za manispaa kinachorudi katika kuboresha miundo mbinu ya masoko na huduma zingine katika utendaji wa masoko

“Takukuru imebaini uwepo wa wafanyabiashara wapatao 234 katika soko la CDT ambao hawalipi kodi au ushuru kwa manispaa ya hivyo kuchangia kushuka kwa Mapato ya manispaa” Amesema Kessy

Aidha Kessy amesema hatua zinazopaswa kuchukuliwa na manispaa ya Kahama ni pamoja ,ukusanyaji wa fedha na Michango kukusanya na kamati au watendaji wa manispaa,kutoa elimu kwa kamati za masoko,manispaa Kufanya ukaguzi upya wa mifumo wa upangishaji vinda na meza”

“Watumishi wa manispaa na watumishi wanaohusika na usimamizi na uendeshaji wa masoko na wahasibu wa Mapato wapewe elimu juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili na kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuinua Mapato ya manispaa” Amesema Kessy.

Amesema Takukuru pia ilifanya uchambuzi wa mfumo wa ugawaji wa madawa hospitali ya wilaya,vituo vya afya na zahanati manispaa ya Kahama na kubaini watumishi wa afya kutojaza kumbukumbu za ununuzi na ugawaji wa dawa,madawa zilizokwisha muda,vituo vya afya kukosa mzigo wa dawa licha ya MSD kukata fedha,ukosefu wa watalamu katika utoaji wa dawa na vifaa tiba.

Katika hatua nyingine amesema pia walifanya ufuatiliaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 158 yenye thamani ya Shilingi Bil.3.3 (3,160,000,000/=) na haijabaini dosari mpaka sasa ambapo ufuatiliaji bado unaendelea, na kubaini Dosari kwenye ujenzi wa miundombinu ya Barabara.

“Mradi wa barabara ya mjini-Old Shinyanga inayotekelezwa chini ya usimamizi wa TANROADS,wenye thamani ya sh.700,010,000/= tulibaini kuwa kifusi cha subgrade layer G15 na sub base Course G25 (stabilized with cement) kimelipwa kwa urefu wa 1,080m badala ya 1,000m na kufanya mkandarasi kulipwa pesa ya ziada ya sh.12,240,000/= kwa kazi ambazo hazijafanyika,hali ya barabara ya mchepuo (diversion Road) siyo nzuri na inaathiri watumiaji”amesema Kessy.

“Ofisi ilifanya mawasiliano na meneja wa mradi TANROAD ambapo alitolea ufafanuzi kuwa wakati wa malipo walijulisha kazi ya barabara za mchepuo (access road/fider road) ambazo mkandarasi atazifanya mwishoni mwa mradi na kuahidi kuzingatia ushauri na kwa sasa barabara imerekebishwa na inapitika”ameongeza.

“TAKUKURU inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali,kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa ubora,kama mtaona kuna vitendo vyovyote vinavyoonesha ubadhilifu vitoe taarifa”amesema.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464