WiLDAF KUWASOMESHA MABINTI VETA BURE WATIMIZE NDOTO ZAO, WAONDOKANE NA UTEGEMEZI

WiLDAF kuwasomesha mabinti VETA bure watimize ndoto zao, waondokane na utegemezi

Na Marco Maduhu, KISHAPU

SHIRIKA la Women in Law and Development in Afrika (WiLDAF), limetoa ufadhili wa kuwasomesha mabinti bure ambao ni Rika balehe na wanawake vijana waliozaa katika umri mdogo, katika vyuo vya ufundi Stad (VETA) ili wapate ujuzi na kutimiza ndoa zao na kuondokana kuwa wategemezi.

Shirika hilo la WiLDAF linatekeleza mradi wa Chaguo langu haki yangu kwa mabinti hao, wakifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) na Finland, kwa lengo la kuwainua kiuchumi, ambapo wakipata ujuzi kutoka VETA watajiajiri na kuchikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Mkuu wa kitengo cha Program kutoka Shirika la WiLDAF Rehema Maro, amesema Mabinti ambao wanawasomesha vyuo vya Ufundi Stad (VETA) wanatoka katika wilaya Tatu ambazo ni Kishapu, Kahama na Butiama wapatao 290, ambapo 240 watasome VETA Kishapu na Shinyanga, na 50 VETA ya Kahama.

“WiLDAF tulianzisha program hii ya chaguo langu haki yangu ili kusaidia mabinti Rika Balehe na wanawake vijana ambao walizaa katika umri mdogo, kwa lengo la kuwapatia ujuzi ambao utawafanya watimize ndoto zao na kuacha kuwa tegemezi,”amesema Maro.

Aidha. amesema mradi huo ni endelevu na mabinti hao wakihitimu watakuja wengine huku wakitoa wito kwa wazazi kuacha kuwaficha mabinti zao wenyewe ulemavu, sababu kipindi wanatafuta mabinti wa kuwasomesha VETA walipata ugumu kuwapata wenye ulemavu ambao na wao wanahaki ya kusoma na kutimiza ndoto zao.

Naye Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo ya kukabidhi mabinti kusoma Chuo cha VETA wilayani Kishapu, Ofisa Maendeleo ya Jamii wilayani humo Joseph Swalala, amewataka mabinti hao kuwa fursa waliyoipata wasiichezee bali wajifunze kwa bidii ili wapate ujuzi ambao utakuwa mkombozi wa maisha yao.

Nao baadhi ya Mabinti hao akiwamo Ester Jovani kutoka wilayani Kishapu, waliahidi fursa hiyo waliyoipata wataitumia vizuri kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao, huku wakilishukuru Shirika la WiLDAF kwa kuwainua sababu walikuwa hawana matumaini tena ya kusoma.

Mkuu wa kitengo cha Program kutoka Shirika la WiLDAF Rehema Maro akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Mabinti Chuo cha VETA Kishapu.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Mabinti kusoma Chuo cha VETA Kishapu.

Mkuu wa Cho cha VETA Shinyanga Magu Mabele akitoa Nasaha kwa Mabinti hao.

Ofisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Prisla Mushi akitoa Nasaha kwa Mabinti hao.

Afisa Elimu Sekondari wilayani Kishapu David Mashauri akitoa Nasaha kwa Mabinti hao.

Binti Ester Jovan akitoa shukrani kwa Shirika la WiLDAF kuwasomesha bure VETA kwa ajili ya kupata ujuzi na kutimiza ndoto zao.

Mabinti wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa kusoma bure katika Chuo cha VETA Kishapu ili watimize ndoto zao.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464