TAKUKURU; AZAKI KAHAMA HAZITOI TAARIFA YA FEDHA KWA HALMASHAURI CHINI YA MIL 20 AMBAZO WANAPOKEA KUTEKELEZA MIRADI

Na mwandishi wetu.

Uchambuzi wa mfumo kuhusu utekelezaji wa mianya ya rushwa kwa asasi za kiraia Manispaa ya Kahama uliyofanya na Takukuru mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha oktoba –desemba ,2022  umebaini AZAKI hazitoi taarifa kwa Halmashauri ya manispaa ya Kahama juu ya fedha chini ya milioni 20 ambazo wanapokea kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy amesema hayo Leo February,16,2022 katika uwasilishaji wa taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 ya kipindi cha oktoba –desemba,2022 kwa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga.Mkuu wa Takukuru mkoa Dionis Kessy akiwasilisha taarifa

Kessy amesema,Hakuna ushirikiano mzuri kati ya Mratibu msaidizi wa Halmashauri ya manispaa ya Kahama na AZAKI kuhusu uwazi wa miradi inayotekelezwa ambapo AZAKI hazito taarifa za mapokezi ya fedha chini ya milioni 20.

Pia Kessy amesema Halmashauri hazitengi bajeti kwa waratibu wa ndani ili kuweza kufatilia miradi inayotekelezwa na AZAKI.

“AZAKI za manispaa ya Kahama hazitoi taarifa za mapokezi ya fedha chini ya milioni 20”amesema Kessy.

Aidha Kessy, alibanisha hatua mbambali zilinazopaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kuondoa changamoto zilizopo baina ya Mratibu msaidizi na AZAKI ikiwa ni uandaji wa kanzidata za NGO ili kufatilia ,AZAKI zitoe taarifa za fedha kwa mratibu wa manispaa ya Kahama.

Takukuru mkoa wa Shinyanga iliweza kushauri ,Halmashauri ya manispaa ya Kahama kuanza hatua za kutenga bajeti kwa ajili ya Mratibu wa manispaa ili kuweza kusimamia AZAKI.

“Kuaniza mwaka wa fedha ujao,Mratibu wa manispaa atanza kupewa bajeti kwa ajili ya kusimamia miradi ya AZAKI”amesema Kessy.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464