MWANDISHI WA HABARI MKONGWE SHABAN ALLEY AELEKEZA NGUVU KWENYE UFUGAJI KUKU NA SAMAKI

 

Mwandishi wa Habari Mkongwe Shaban Alley amezindua Jina la Kampuni ya Uzalishaji wa Kuku na Samaki ‘Alle Fish & Poultry Farm' dhamira kuu ikiwa ni kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji katika Manispaa ya Shinyanga.

Alley ambaye anajishughulisha ujasiriamali kwa ufugaji wa kuku na samaki katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga amesema matarajio yake makubwa mwaka 2023 ni kuongoza zaidi uzalishaji wa kuku wa nyama na mayai lakini pia samaki.


“Mwaka huu 2023 tutaanza uzalishaji wa vifaranga vya kuku wa nyama na mayai lengo ni kuongeza uzalishaji wa kuku wa kienyeji ambao mahitaji yake ni makubwa zaidi. Tumeamua kufanya hivi baada ya kubaini kuwa kuku wa kienyeji wanatoweka”,amesema Alley.


Hata hivyo amesema kwa Sasa wafugaji wanakabiliwa na changamoto ya mfumko wa bei ya dawa na chakula cha kuku hali ambayo inasababisha baadhi ya wafugaji kushindwa kuendelea na ufugaji.


“Tunaomba serikali kuangalia njia ya kukabiliana na mfumko wa bei  kwani changamoto inayotukabili ni gharama kubwa ya dawa na chakula cha kuku na samaki”,amesema Alley.


 Aidha Alley ameishukuru serikali kudhibiti uingizwaji holela wa vifaranga vya kuku kutoka nje ya nchi hali iliyokuwa inazorotesha ufugaji wa ndani ya nchi


Wasiliana na Shaban Alley kwa simu namba 0754680089

Mjasiriamali/Mwandishi wa Habari Mkongwe Shaban Alley akilisha kuku
Mjasiriamali/Mwandishi wa Habari Mkongwe Shaban Alley akizungumza na mwandishi wa habari

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464