MILANGO YA BIASHARA IMEFUNGUKA SOKO LA NCHI ZA AFRIKA - ALLY GUGU


Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ndg. Ally Gugu (Uwekezaji) akifungua Warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023
Washiriki mbalimbali wa warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023.
Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ndg. Ally Gugu (Uwekezaji) katika na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Ndg. Gielead Teri katika ufunguzi wa Warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023.
***

Serikali inaandaa mkakati maalum kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa kutuongoza na kuchanganua vipaumbele katika kuratibu na kushiriki soko huru barani Afrika.


Hayo yamesemwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na biashara Ndg. Ally Gugu, wakati akifungua warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la biashara la nchi za Africa katika ukumbi wa Hoteli ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023


“Serikali imelenga kutoa elimu na ufafanuzi zaidi kwa Sekta binafsi na wafanyabiashara ili kupanua uelewa wa bidhaa na huduma ambazo zinahitajika zaidi katika soko la nchi za Afrika”,amesema Gugu.


Ndg. Gugu amesisitiza uhamasishaji na utekelezaji wa ajenda ya Afrika tunayoitaka ambapo biashara ni moja ya ajenda kuu


“Soko hili ni la watu bilioni 1.2 ambapo jana Nchi ya Comorro imeweza kuridhia ushiriki wake katika soko huru barani Afrika”. Ameongeza Gugu


Benki ya Maendeleo ya Afrika na AfriExim zimejitokeza katika kusaidia washiriki mbalimbali watakaopenda kupata huduma za kifedha ili kuwezeshwa kushiriki katika biashara kwenye soko huru barani Afrika.


Tanzania chini ya usimamizi wa Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia itifaki za kushirikisha wanawake na vijana katika soko hilo na tayari mkutano mkubwa wa kushirikisha vijana na wanawake ulifanyika Septemba 2022 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan aliongoza viongozi mbalimbali katika mkutano huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464