MRADI WA VYOMBO VYA
HABARI SHINYANGA, WALETA MATOKEO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NA KUEPUSHA
WANAFUNZI KUTEMBEA UMBALI MREFU.
Majengo ya madarasa ya shule ya sekondari ya luhumbo iliyoka kata ya didia.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 waliopokelewa katika shule ya sekondari luhumbo.
Diwani wa kata ya Didia ,Luhende Masele akiongea na vyombo vya habari kuhusu matokeo ya ujenzi wa shule kwa nguvu za serikali na wananchi.
Serikali na wananchi wa kata ya didia wafanikiwa kuanzisha shule ya sekondari Luhumbo kwa ajili ya kunusuru watoto wanaotembea umbali mrefu zaidi ya kilomita nane(8) kila siku baada ya juhudi za pamoja zilizoanza toka mwezi machi,2021 baada ya vyombo vya habari kupaza sauti ya uwepo wa matukio ya ukatili unaosababishwa na wanafunzi kutembea na umbali mrefu.
Ukamilishaji wa shule
ya sekondari Luhumbo katika kata ya didia umetokana na Klabu ya Waandishi wa
Habari Mkoa wa Shinyanga kupaza sauti kupitia mradi wa “Nafasi ya vyombo vya
habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto” uliotekeleza kwa
kipindi cha januari hadi machi,2021 na kwa ufadhili wa Mfuko wa wanawake Tanzania
(Women Fund Tanzania) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Shinyanga imefanya ufatiliaji wa matokeo ya mradi huo februari,2023
na kubaini jamii na serikali kufanikiwa kujenga madarasa manne na matundu kumi
na mbili ya vyoo kwa jumla ya Tshs million 95 ambapo serikali imegharamia kwa
Tshs million 80 na wananchi kwa Tshs milioni15.
Shule ya sekondari
luhumbo imefanikiwa kupokea wanafunzi 135(ME-74, KE-61) kwa mwaka 2023 na
kusaidia wanafunzi kuepuka umbali wa kilomita 8 kwenda hadi shule ya sekondari
didia.Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Didia ,Bwana Luhende Masele wakati
akiongea na vyombo vya habari,Februari 8,2023.
Diwani wa kata ya didia,
Luhende Masele alisema,Tumefanikiwa kupunguza utoro na kuokoa watoto kutembea
umbali mrefu zaidi ya kilomita 8 na kuwaepusha na matukio kadhaa ya vitendo vya
ukatili ikiwa ni kubakwa,mimba za utotoni na hata kutishiwa na wanyama wakali
wakati wa jioni na asubuhi.
Masele
alisema,Tumefanikiwa kwa hatua za awali kuwa na sekondari hii kwa eneo letu na
tumebaki na changamoto ya maabara na ofisi ya waalimu na tunayo mipango ya
kuweka juhudi za pamoja tena ili kuweza kukamilisha na hata kuweka ukuta kwa
ajili ya usalama na ulinzi wa wanafunzi.
“Wadau wa ukatili kwa
kushirikiana na vyombo vya habari waliweza kuibua habari matokeo katika dhamira
ya kupinga ukatili kwa kupaza sauti.Jamii ilipokea mrejesho baada ya sauti ya
vyombo vya habari na ikaweka mipango ya kutenga eneo la hekari 10 ili kuweza
Kujenga shule ili kusaidia wanafunzi”Alisema Masele.
“Mimi kama kiongozi wa
kata,nilipokea mrejesho na kuweza kutumia jukwaa la baraza la madiwani la
Halmashauri kuweza kupeleka hoja ya wananchi na kushawishi serikali kuweza
kutupatia rasilImali fedha ili kuweza kukamilisha ujenzi wa shule hii na ambapo
serikali iliridhia na kutupatia kiasi cha Tshs million 80 na kutupa jukumu la jamii kukamilisha miundio
mbinu ya matundu ya vyoo vya shule,Jamii ilishiriki kwa nguvu zao na michango
ya fedha kwa kiasi cha Tshs million 15” Alisema Masele.
Aidha Afisa Elimu wa
Kata,Justus C.Birago, Alisema tulijadili suala hili kupitia vikao vya kata na
tumefanikwa kupata shule ya wanafunzi 135 kwa mwaka huu kutoka katika kata na
kusaidia watoto kutotembea kilomita 8 hadi shule ya sekondari didia iliyoko kijiji cha bukumbi.Jamii iliweza kutenga eneo la ekari 10 kwa manufaa ya watoto wao.
“Tunashukuru serikali
na wadau kwa hatua za awali za kuleta matokeo katika elimu kwa kata hii na vema
basi tuwe pamoja katika ukamilishaji wa chumba cha waalimu na
maabara.Tumeshuhudia nguvu vya vyombo vya habari katika utekelezaji wa mradi
wao kwa matokeo ya shule hii kuwepo na kutoa huduma”Alisema Birago
“Kupitia vikao vya
ODC,tuliomba serikali kuelekeza fedha za UVIKO zitumike kujenga madarasa manne
ya shule katika eneo letu kutokana na changamoto iliyopo na walikubali na
walituagiza tuishirikishe jamii kukamilisha sehemu ya matundu ya vyoo na chumba
cha maabara”Alisema Birago
Kwa upande wake, Juma L.Kisenha,Makamu
wa shule hiyo,Alisema hadi leo februari 8,2023 wanafunzi walipokelewa ni 136
kwa wanaotoka ndani ya kata hiyo na anashukuru serikali kwa sehemu kubwa ya
kuweka nguvu ya ujenzi wa madarasa hayo.
Baadhi ya wanafunzi walioongea
na vyombo vya habari, walidai imesadia wao kutotembea umbali mrefu na kuwaepusha
na vitendo vya ukatili.
“shule imetusaidia
kutotembea umbali mrefu na hasa wasicha watakwepa vishawishi kutoka kwa makundi
ya mitaani ya vijana.” Alisema Petro Masunga (18)
“Naishukuru serikali
kwa kutujengea shule hii na itatusaidia kutotembea umbali mrefu wa kwenda kule
shule ya sekondari didia”Alisema Magreth Robert(13)
“Hii itatusaida hata kupanda kitaalum na kuwa hatutaweza kuchoka sana kwa kutembea umbali mrefu zaidi” Alisema Erick Salu shija(16)
Magesa Faustine mkazi wa kata ya didia ,alisema vyombo vya habari vimeleta matokeo ya uwepo makubwa ya kuweza kutatua changamoto ya watoto wetu kutembwa umbali mrefu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464