Naibu Waziri
wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul amewataka maafisa michezo na
maafisa utamaduni kuanzia ngazi ya Wilaya kuhakikisha wanazitembelea shule za
msingi na sekondari ili kuona kama wanapata muda wa kushiriki kwenye michezo
ili kuimarisha afya na kujiepusha na magonjwa.
Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul ametoa agizo hilo February 18 alipotembelea
shule ya sekondari Don Bosco Kata ya Didia Halmashauri ya Shinyanga na
kushiriki tamasha la michezo lililoandaliwa na shule hiyo ambalo hufanyika kila
mwaka.
Naibu Waziri
Gekul ameipongeza shule ya Don Bosco kwa kuwa na utaratibu wa kuandaa matamasha
ya michezo ambayo yanasaidia kuimarisha afya kwa walimu na wanafunzi na
kuwawezesha kusoma vizuri bila kusumbuliwa na magonjwa.
“Nimefurahi
sana kuona wanafunzi wanacheza michezo mbalimbali hii inaonesha wazi hata afya
zao ziko vizuri,pia nimefurahi kuona mna kiwanja kizuri kwa ajili ya
michezo,sasa natumia fursa hii kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini ambazo
hazina viwanja kutenga maeneo ya viwanja vya michezo” amesema, Gekul.
Naibu Waziri
amewataka maafisa michezo na maafisa utamaduni kuhakikisha wanakagua viwanja
vya michezo kama vina miundombinu inayotakiwa ili kuwawezesha watumiaji kufanya
mazoezi bila kuwa na changamoto.
Katika hatua
nyingine Naibu Waziri amewataka wanafunzi kujiepusha na makundi ambayo yanaweza
kuharibu ndoto zao kutokana na kwamba maadili yameporomoka katika jamii huku
akisisitiza suala la kuwa na hofu ya Mungu na kuzingatia kilichowapeleka shule
kupata elimu ili kutimiza malengo yao.
"Pamoja na kuhamasisha michezo lakini mimi kama mama yenu ni lazima nitoe
nasaha kama mzazi,maana suala la maadili limekuwa ni tatizo kubwa wapo mabinti
wanakatisha ndoto zao kwa kupata ujauzito na kukatisha ndoto zao amsijiingize
kwenye mahusiano zingatieni masomo'' amesema Naibu Waziri.
Mwalimu wa michezo shule ya Sekondari Don Bosco Zipapa James amesema michezo imesaidia kujenga undugu na urafiki pamoja na kuimarisha afya kwa wanafunzi na walimu na kuwawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Don Bosco Kata ya Didia akimvisha skafu Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul baada ya kuwasili katika shule hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Felix Wagi akizungumza wakati wa tamasha la michezo
Wanafunzi wakionesha michezo mbalimbali
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464