Mwenyekiti wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group Shinyanga (EVAWC WG) Jonathan Manyama akizungumza kwenye kikao cha robo mwaka kilichofanyika mjini Shinyanga.
Suzy Luhende, Shinyanga Blog
MWENYEKITI wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group Shinyanga (EVAWC WG) Jonathan Manyama amewataka wajumbe wa Working Group kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Hayo amesema leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Evawc uliofanyika mjini hapa, ambapo amewataka wajumbe wote kuwa na umoja na nguvu moja ili kuhakikisha wanatokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
"Niwaombe ndugu zangu tuone hiki chombo ni cha thamani sana tunapokutana tushirikiane kikamilifu wote kwa nguvu moja katika kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,tukiwa pamoja na tufanye kazi zetu kwa amani ili kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto,"amesema Manyama.
"Lengo la group hili ni kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, hivyo hatuko tayari kulea mtu ambaye yuko kinyume na sisi anatukosea heshima, tunataka mtu anaetoa ushirikiano wa kutokomeza ukatili, kwani kuna watoto wanafanyiwa ukatili na kuna wanawake wanafanyiwa ukatili tuwasaidie tuelimishe jamii iachane na ukatili wa aina yeyote,"amesema Manyama.
Kwa upande wake mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia amewataka waendelee kushirikiana katika kufanya kazi zao kwa amani kabisa wasiwasikilze watu ambao wanaweza kuvuruga kikundi hicho.
"Endeleeni kujifunza na kuangalia wapi hamjafanya, wafikieni wananchi muwaelimishe waondokane na mila potofu ukatili kwa watoto na wanawake na mfanye kazi zenu kwa amani kabisa muendeleze nguvu ya pamoja ili kuhakikisha mnatokomeza ukatili wa kijinsia, kwani inawezekana,"amesema Mbia
Katibu wa Evawc Piter Amani amesema kwa sasa group hilo lina wajumbe 26 na lengo la group hilo ni kuelimisha jamii na kushughulikia watu ambao wameshafanyiwa ukatili wa kijinsia na kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha Veronica Masawe kutoka Shirika la Women young Leadership (WYL) akishirikiana na Estomine Henily kutoka ofisi ya waandishi wa habari Shinyanga Press Clabu katika kitengo chao wamefungua Instagrame yenye logo ya EVAWC hivyo watu wote wanawakaribisha
kufungua na kushea kwa watu mbalimbali ili waweze kusoma kilichomo lengo ni kutokomeza ukatili.
"Pia tuko mbioni kufungua facebook, twitter pamoja na you tubu ili kuhakikisha tunawifikia watu wote na ukatili wakijinsia tunautokomeza kabisa usiendelee kuwepo,"amesema Veronika Masawe.
Wajumbe wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group Shinyanga (EVAWC WG) wakiwa kwenye kikao
Katibu wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group Shinyanga (EVAWC WG) akizungumza kwenye kikao hicho
Mjumbe wa Shinyanga Ending Violence Against Working Group Shinyanga (EVAWC WG) akiwasilisha kazi za group hilo
Mjumbe Zengo akichangia jambo kwenye kikao hicho
John Shija kutoka Shirika la Paceshi akichangia jambo kwenye kikao hicho
Pendo Sawa kutoka wanawake laki mojaakiwa kwenye kikao hicho
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464