Wanawake wachimbaji wadogo wa madini kikundi cha Mshikamano
(Tawoma) katika mgodi wa Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala
Wilayani Kahama,wamejenga jengo la zahanati kijiji cha Nyamishiga hatua
itakayosaidia kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi na kuwaondolea adha
ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu Lunguya.
Mwenyekiti wa wachimba wa madini wanawake Tanzania,ambaye
pia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano Tawoma mgodi mdogo wa Nyamishiga
Semeni John,amesema ujenzi wa zahanati hiyo pamoja na nyumba ya Daktari fedha
zake zinatokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini wanawake ambazo
zinakwenda kusaidia huduma za jamii.
Amesema tayari Sh Milioni 203 zimetolewa na wanawake
wachimbaji wa madini ambazo zinatumika kwenye ujenzi wa zahanati,vyoo,na nyumba
ya Daktari hatua ambayo itasaidia kupunguza changamoto zilizopo kutokana na
Kijiji hicho kutokuwa na huduma za afya ambapo wananchi wanalazimika kutembea
umbali mrefu kwenda kituo cha afya Lunguya.
“Tangu tumeanza usimamizi wa mgodi huu sisi wanawake
tumeiingizia mapato serikali zaidi ya Sh Bilion mbili ambapo pia tumejenga
zahanati itakayosaidia kutoa huduma kwa wananchi,na wachimbaji wadogo wa madini
ambao wengi wako katika eneo hilo wakiendelea na shughuli zao za kila
siku”alisema Semeni John Mwenyekiti wa Tawoma.
Katibu wa Kikundi cha Tawoma Hilda Busomelo amesema zahanati
hiyo atasaidia wakina mama wajawazito na watoto kupata huduma karibu badala ya
kutembea umbali mrefu kupeleka watoto kliniki na kwenda kwenye matibabu.
Amesema mbali na kusaidia huduma za jamii lakini pia
wamekuwa wakitoa msaada kwa wazee wasiojiweza ili kuwawezesha kujikimu kimaisha
pamoja kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Wanawake hao wachimbaji wadogo wa madini pia wameiomba serikali
kupitia wizara ya madini kuwarasimisha na kuwapatia leseni za uchimbaji mdogo
kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji
wa mapato ya serikali.
Baadhi ya viongozi wa wachimbaji wa madini wanawake