AFISA LISHE MSALALA AWAFUNDA WANAWAKE UJAUZITO UNAPATIKANA KWA MAANDALIZI





 Afisa lishe wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga akitoa Elimu ya Lishe kwa wanawake katika siku ya maadhimisho ya wanawake duniani

Na Kareny Masasy, Msalala

BAADHI ya  wanawake kutoka  kata ya Mwakata halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameelezwa ili kupata mtoto aliyebora na sio bora mtoto wahakikishwe wanafanya maandalizi ya kubeba ujauzito.

Wapo akina mama wengine wakiulizwa baada ya kuona hakufanya maandalizi ya ujauzito anadai imekuja kwa bahati mbaya  ndiyo hapo badaye yanapoibuka  matatizo kwenye afya ya uzazi na mtoto.

Afisa lishe wa halmashauri hiyo  Peter Ngazo amesema hayo  jana katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani huku akieleza maandalizi yafanyike kabla ya miezi sita ya kutaka kupata mtoto.

“Maandalizi hayo katika ujauzito yatamuepusha mama kuugua, kukosa upungufu wa madini chuma na damu ,kuwa na uwezo wa kupata mtoto bora asiye na maradhi”amesema Ngazo.

Ngazo amesema wapo baadhi ya wanawake wanaopata ujauzito kwa madai hawakutarajia  na mahudhurio ya kliniki mpaka afikishe miezi mitano au saba hiyo unajihatarishia maisha mwenyewe ukihisi unaujauzito wahi kliniki.

 Ngazo amesisitiza unyonyeshaji wa miaka miwili kwa mtoto kwani robo tatu ya maziwa ya mama ni maji na sehemu inayobaki  ni virutubisho ndiyo maana unaelezwa kitaalamu mtoto usimpe kitu chochote hata maji muda wa miezi sita mfululizo.

Ngazo anasema mtoto anapozaliwa  tu anatakiwa kunyonyeshwa ili kuweza kupata virutubisho vya kinga mwilini na kufanya mifumo ya fahamu kufunguka.

Ngazo amesema wazazi wanatakiwa kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kuwa na uzazi wa mpango ili kutoa nafasi ya mtoto kunyonya muda wa miaka miwili  inayoelezwa na wataalamu kliniki.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464