BENKI YA TADB, HEIFER INTERNATIONAL WAENDESHA MKUTANO WA WADAU SEKTA YA MAZIWA SHINYANGA

Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga ukiendeshwa wa HEIFER International na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Shirika la HEIFER International wameendesha Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika leo Machi 22, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa maziwa pamoja na viongozi wa Serikali wakiwamo maofisa ugani, huku Mgeni Rasmi akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme.

Akizungumza kwenye Mkutano huo Mratibu wa Mradi wa (TI3P) wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula, amesema benki hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kuleta maendeleo katika Sekta ya Kilimo na kuhakikisha nchi ina jitosheleza katika suala zima la upatikanaji wa chakula pamoja na kusaidia wakulima wadogo kuondokana na uzalishaji wa kujikimu bali wafanye na kilimo biashara.

Amesema Benki hiyo iliona kuna fursa katika Sekta ya Maziwa kwamba kumekuwapo na mwamko wa watu ambao wanahitaji kunywa maziwa ambayo ni salama na pia matumizi ya maziwa yanapunguza utapiamlo kwa watoto na kuimarisha afya na pia Sekta hiyo inaiunua kipato cha wafugaji.

Amesema zaidi ya 80 ya wafugaji wanaozalisha maziwa ni wafugaji wadogo hivyo wakaona ni vyema wawaendeleze na hatimaye kuja na mradi wa kuendeleza Sekta ya ndogo ya Maziwa, Mradi ambao ni shirikishi wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa Tanzania (TI3P) ambao ulizinduliwa mwaka jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao ni wa miaka mitatu.

“Mradi huu umelenga zaidi kutatua changamoto ambazo zinawakabili wasindakaji wa maziwa ili mwisho wa siku wanufaike na Mnyororo wa thamani katika Sekta ya Maziwa, na unatekelezwa katika maeneo mawili ya Kanda ya Ziwa pamoja na Zanzibar,”amesema Mabula.

Aidha, amesema mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na wadau wa HEIFER International ambao ni wataalam na wanauzoefu mkubwa katika Sekta ya Maziwa, na zimetengwa dola milioni 40 ambazo zitaingia katika kuinyanyua Sekta hiyo ya maziwa na kupewa wafungaji fursa ya kokopa kupitia vikundi,”ameongeza.

Naye Mwakilishwa wa Mkurugenzi Mkazi wa HEIFER International Nyamate Musobi ambaye ni Afisa Uendeshaji, amesema kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo wapo Kanda ya Ziwa kutekeleza mradi Shirikishi wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa na wanauzoefu wa muda mrefu tangu mwaka 1974, na wamekuwa wakifanya kazi sana Nyanda za juu Kusini na Kaskazini.

Amesema na sasa wamekuja kutekeleza mradi huo Kanda ya Ziwa eneo ambalo halijaendelezwa na limekuwa na changamoto katika uzalishaji, miundombinu ya ukusanyaji wa maziwa hata masoko ya maziwa Kanda ya Ziwa ipo chini, hivyo kupitia mradi huo wamekuja kuleta mabadiliko.

“HEIFER tumejulikana kwa mradi wa kopa Ng’ombe lipa Ng’ombe, moja wapo la Shirika ambalo limesaidia watanzania kuwa na Ng’ombe wengi wa maziwa na tulileta Ng’ombe zaidi ya Laki Mbili na tumechangia uzalishaji mkubwa wa maziwa,”amesema Nyamate.

Amesema pia katika mchango wao wa kukuza Sekta ya Maziwa waliweza kuwaweka wafugaji pamoja kwenye vikundi na kuendeleza Tasnia ya Ushirika na kuunda vyama vya Ushirika zaidi ya 60 na wamefanya kazi za vyama vya ushirika zaidi ya vyama 119 huko walipotoka.

“Katika utekelezaji wa mradi huu tutakuwa na majukumu makubwa matatu, na jukumu la kwanza ni kuhakikisha wafugaji tunawaweka pamoja, kuwajengea uwezo kuanzia kwenye vikundi ili wapate mafunzo mbalimbali na kuongeza uzalishaji, kuwasaidia ziwe taasisi za kibiashara kwa kushirikiana na tume ya maendeleo ya ushirika, kuwaunganisha na wanunuzi mbalimbali, na kuboresha miundombinu ya ukusanyaji wa maziwa,”amesema Nyamate.

Katika hatua nyingine amesema kipindi wanafanya tathimini kabla ya kufanya utekelezaji wa mradi Kanda ya Ziwa ushiriki wa akina mama katika kunufaika na Mnyororo wa Thamani wa Maziwa upo chini sana, na kubainisha changamoto waliyoibaini akina mama hawana Rasilimali za Mifugo na kupitia mradi huo wataona namna ya kusaidia akina mama kupata Rasilimali hizo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambao ndiyo watekelezaji wakuu wa mradi na kushirikiana pia na Halmashauri kupitia Ofisi za Maendeleo ya Jamii.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo wa Shinyanga, amesema mradi huo utaleta chachu ya mabadiliko na kuongeza uzalishaji na ukusanyaji wa maziwa katika vituo Rasmi pamoja na kuongeza pato la wafugaji wadogo na taifa kwa ujumla.

Amesema Sekta ya Maziwa ina mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya Mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na kutaja mchango huo kuwa ni kuimarisha upatikanaji wa lishe bora kwa watoto, kuboresha afya za wananchi, kupunguza umaskini kwa wafugaji, kupunguza uingizwaji wa maziwa kutoka nje ya nchi, na kuongeza makusanyo ya Serikali sababu Sekta hiyo inachangia asilimia 2.3 ya pato la taifa.

Ametaja faidi zingine ni kuchochea ukuaji wa Sekta ya Viwanda vya kusindika maziwa kutokana na uwepo wa malighafi.

Aidha, ametoa maelekezo ya msisitizo katika kukuza Sekta hiyo ya Maziwa kuwa Halmashauri zihakikishe zinatenga maeneo ya kwa ajili ya malisho, kuimarisha miundombinu ya maji na uchibwaji wa mabwawa, Majosho pamoja na Maofisa ugani kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa.

Amesema halmashauri ziendelee kuhamasisha unywaji wa maziwa Maofisini na kushirikiana na TAMISEM kuendeleza mpango wa unywaji wa maziwa shuleni ikiwamo kupitia mikataba na wasindikaji wa maziwa na kusambaza maziwa kwenye shule zote zilizopo katika maeneo yao.

Afisa uzalishaji wa Maziwa kutoka Bodi ya Maziwa Deogratias Buzuka, amewataka Wananchi watumie maziwa ambayo yamesindikwa kuwa ndiyo yapo salama, na wakitumia maziwa ambayo hayapita kwenye mfumo Rasmi ni kujitafutia magonjwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Mratibu wa Mradi wa TI3P kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula akielezea mradi huo kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maziwa.
Afisa Uendeshaji Mradi wa HEIFER International Nyamate Musobi akielezea utekelezaji wa mradi wa TI3P kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB.
Mratibu wa Mradi wa TI3P kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula akiwasilisha maelezo ya Tasnia ya Maziwa Tanzania kwenye Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Afisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka HEIFER International Willifaston Ntoroma akiwasilisha jinsi ya utekelezaji wa Mradi.
Afisa Uzalishaji wa Maziwa kutoka Bodi ya Maziwa Deogratias Buzuka akizungumza kwenye Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Meza Kuu wakiwa kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga (kulia) Beda Chamatata, akiwa na Afisa Uendeshaji wa HEIFER International Nyamate Musobi kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, (kushoto) akiwa na Afisa Uendeshaji Mradi wa HEIFER International Nyamate Musobi wakifuatilia mawasilisho na uchangiaji wa mada kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa kikiendelea mkoani Shinyanga.
Washiriki wakiwa kwenye kikao cha Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada kumalizika kwa Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464