Amefanya ziara hiyo jana Machi 22 2023.
Mhe. Mkude amesema lengo la ziara hiyo ni kufanya ukaguzi katika sehemu za kuhifadhia vifaa vya ujenzi pamoja na mafuta kutokana na matukio ya wizi ambayo yanaendelea katika mradi wa SGR“Tulikuwa tukipata ripoti za mara kwa mara juu ya matukio ya wizi wa vifaa vya ujenzi kama vile Saruji, nondo na mafuta kwa wingi sana, sasa tukaona tufatilie ili tubaini kama kuna mapungufu ili tuweze kushauri yarekebishwe,” amesema Mkude.
Pia Mhe. Mkude amekiri kuwepo kwa mapungufu makubwa kwenye baadhi ya maeneo ya stoo katika mradi wa ujenzi wa reli ya SGR ikiwemo kutokuelewana kwa lugha kati ya Wachina na vibarua.